Mwanahabari wa Marekani kufikishwa mahakamani Urusi kwa tuhuma za ujasusi

 

Mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich atashtakiwa nchini Urusi kwa mashtaka ya ujasusi, waendesha mashtaka wa Urusi wamesema.

Ripota wa Wall Street Journal ameshutumiwa kwa kukusanya "taarifa za siri" kutoka kiwanda cha kutengeneza vifaru cha Urusi kwa niaba ya CIA.

.

Waendesha mashtaka wanasema atasimama katika mahakama ya Yekaterinburg - mji aliokamatwa mwezi Machi mwaka jana akiangazia vita vya Ukraine.

Bw Gershkovich, gazeti lake na Marekani zinakanusha mashtaka, huku Washington ikimtaja rasmi kama "aliyezuiliwa kimakosa".

Waendesha mashtaka wa Urusi walisema siku ya Alhamisi kwamba uchunguzi ulibaini kwamba mwandishi huyo alikuwa amekusanya "taarifa za siri" kuhusu "uzalishaji na ukarabati wa vifaa vya kijeshi" kutoka kwa kiwanda cha kutengeneza vifaru cha Urusi.

Katika taarifa, walimshutumu kwa kufanya "vitendo haramu kwa kutumia njia za kula njama".

Hii, waendesha mashtaka walisema, ilikuwa "kwa maagizo ya CIA".

Tangu kukamatwa kwake, Bw Gershkovich amesalia katika kizuizi kabla ya kesi yake kuanza ramsi mjini Moscow, maili 1000 (1609km) kutoka Yekaterinburg.

Amekaa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja na akipatikana na hatia anakabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela.

Kukamatwa kwake kulikua mara ya kwanza kwa Urusi kumshutumu mwandishi wa habari wa Marekani kwa ujasusi tangu enzi ya Usovieti.

Ubalozi wa Marekani mjini Moscow umesema sababu za kuzuiliwa kwake hazina msingi.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo