"Netanyahu ni kichaa; kichaa chake hakitibiki, yeye na mkewe na mwanawe"

 

Baada ya waziri mkuu wa Israel, kutoa amri ya kuuliwa kwa umati na kujeruhiwa Wapalestina 610 kwa mkupuo mmoja, watu wengi wamesisitiza kuwa Benjamin Netanyahu ana maradhi ya kichaa kibaya cha kunusa damu za watu wasio na hatia.

Makala iliyochapishwa na shirika la habari la Mehr inasema kuwa, tangu ulipopandikizwa utawala katili wa Kizayuni katika eneo la Asia Magharibi mwaka 1948, muda wote tumeshuhudia jinai za kutisha na za kiwendawazimu za Wazayuni dhidi ya Wapalestina lakini jinai zinazofanywa hivi sasa na utawala huo pandikizi na katili ni kubwa mno na ni za kutisha kupindukia kiasi kwamba hivi sasa zimezidi kupata nguvu taarifa kuwa waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu anaugua ugonjwa mbaya sana wa wendawazimu. 

Katika sehemu yake moja, makala hiyo imemnukuu Ehud Olmert, waziri mkuu wa zamani wa utawala wa Kizayuni akisema kwenye mahojiano maalumu kwamba, kuna baadhi ya maradhi yanatibika, lakini maradhi ya akili ya waziri mkuu na mkewe na mtoto wake hayatibiki na njia pekee ya kuiokoa Israel ni kupelekwa wagonjwa hao kwenye vituo vya matibabu ya akili. 

Benjamin Netanyahu ana maradhi mabaya ya kichaa

 

Olmert si pekee anayeamini kuwa Netanyahu ana kichaa kibaya sana; yeye na mkewe na mwanawe wa kiume, bali maafisa wengine wa ngazi za juu wa utawala wa Kizayuni akiwemo mbunge wa utawala huo, Ofer Cassif wana yakini kwamba Netanyahu na mkewe na mwanawe wa kiume wanaugua wendawazimu.

Yair Lapid, ni kiongozi mwingine wa utawala wa Kizayuni ambaye amefikia hata kuchukua hatua za kisheria za kuthibitisha kuwa Netanyahu ni mwendawazimu na hafai kuongoza utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa makala hiyo, kuna ushahidi mwingine mbalimbali wa kimaandishi zikiwemo nyaraka za siri za kesi ya Netanyahu na familia yake ambazo zimefichua kuwa watu hao ni wagonjwa wa akili tena wameshiriki kwenye vikao vingi tu vya matibabu ya akili. 

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China