Polisi wa US wakamata waandamanaji 70 baada ya kuvamia ubalozi wa Israel, San Fransisco
Polisi wa Marekani katika mji wa San Fransisco wamewakamata waandamanaji wapatao 70 wanaotetea na kuunga mkono Palestina baada ya kuingia kwenye ukumbi wa ubalozi mdogo wa utawala wa Kizayuni wa Israel ulioko kwenye mji huo.
Mmoja wa waandamanaji aitwaye Sarah mwenye umri wa miaka 54 amesema: "tunafanya hivi kwa sababu sisi ni sehemu ya umati unaoongezeka wa watu wanaotaka kukomeshwa mauaji ya kimbari na ambao wako katika mshikamano na Palestina na wana wasiwasi sana kuhusu ushiriki wa serikali ya Marekani katika mauaji ya kimbari yanayotokea".
Zaidi ya Wapalestina 36,470, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wameshauawa hadi sasa katika vita vya kinyama na mauaji ya kimbari yaliyoanzishwa na jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza kufuatia operesheni ya kulipiza kisasi ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyotekelezwa na harakati za Muqawama wa Palestina za Ghaza Oktoba 7,2023
Tangu vilipoanza vita hivyo, Marekani imekuwa ikiusaidia na kuuunga mkono utawala wa Kizayuni kwa kuupatia maelfu ya tani za silaha na zana za kijeshi ambazo unazitumia kuteketezea roho za Wapalestina wasio na ulinzi.../