Saa 2 zilizopitaChama cha Zuma chadai kuhesabiwa upya kwa kura
Chama cha Zuma chadai kuhesabiwa upya kwa kura
Chama cha Umkhonto we Sizwe (MK) cha Rais wa zamani Jacob Zuma kimewasilisha malalamishi kwa Tume Huru ya Uchaguzi ya Afrika Kusini (IEC)
Huku 98% ya kura zikiwa zimejumlishwa hadi sasa, MK inashindwa kupata wingi wa kura katika ngazi ya mkoa huko KwaZulu-Natal.
Msemaji wa chama Nhlamulo Ndhlela amesema idadi ya IEC hazilingani na walizokusanya mashinani na hivyo wanataka kuhesabiwa upya kwa kura.
Ndhlela ametoa wito kwa wafuasi wa MK kutofanya vurugu.