Saa 2 zilizopita'Wapanga mapinduzi' yaliyoshindwa wafikishwa mahakamani DRC

 

Kesi ya watu 51, wakiwemo Wamarekani watatu, wanaotuhumiwa kujaribu kumpindua rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi uliopita, imeanza.

Kesi hiyo inaoneshwa moja kwa moja kwenye TV na redio ya taifa kutoka jela ya kijeshi ya N'dolo katika mji mkuu, Kinshasa.

Washtakiwa hao walifikishwa katika mahakama ya kijeshi wakiwa wamevalia mashati ya bluu na manjano, ikiwa ni mara ya kwanza kuonekana hadharani tangu mapinduzi hayo kushindwa.

Waliokamatwa wakati wa mashambulizi kwenye ikulu ya rais na nyumba ya mshirika wa Rais Félix Tshisekedi, wanakabiliwa na mashtaka mengi, ikiwa ni pamoja na kufadhili ugaidi, mauaji na jaribio la mauaji. 

Watu hao walikamatwa tarehe 19 Mei katika ikulu ya rais na nyumbani kwa mmoja wa washirika wa Rais Tshisekedi.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema haijapewa fursa ya kuwafikia raia wake walioko kizuizini.

Watu sita waliuawa wakati wa jaribio la mapinduzi tarehe 19 Mei, akiwemo mshukiwa kiongozi wa njama hiyo Christian Malanga.

Washtakiwa wengine walizuiliwa baada ya mashambulizi dhidi ya Palais de la Nation na nyumba ya Vital Kamerhe, ambaye ni spika wa bunge.

Ripoti za vyombo vya habari vya ndani zilisema washambuliaji hao walikuwa wanachama wa Vuguvugu la New Zaire lenye uhusiano na Malanga, mwanasiasa wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye alipata uraia wa Marekani.

Mwanawe Marcel Malanga ni miongoni mwa raia wa Marekani waliokamatwa. Mwingine ni Tyler Thompson mwenye umri wa miaka 21, ambaye familia yake iliiambia BBC wiki hii kuwa "hawakuwa na wazo lolote" jinsi alivyojiingiza katika mpango huo.

Video zilizochukuliwa mjini Kinshasa baada ya tukio hilo zinaonesha Bw Thompson akipigwa na kitako cha bunduki na kupigwa mara kwa mara kichwani na vikosi vya usalama vya Congo.

Watu wengine wa mataifa tofauti pia walihusika na wako mahakamani, kulingana na msemaji wa jeshi Jenerali Sylvain Ekenge.

Mmoja ni raia wa Congo ambaye ana uraia wa Ubelgiji na pia kuna raia wa Canada mwenye asili ya DR Congo

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo