Ukraine yaangusha ndege 23 zisizo na rubani usiku kucha
Ukraine yaangusha ndege 23 zisizo na rubani usiku kucha
Jeshi la wanahewa la Ukraine limesema limeangusha ndege zote 23 zisizo na rubani na makombora matano kati ya sita yaliyorushwa na Urusi asubuhi ya leo.
Serhii Tiurin, gavana wa eneo la Khmelnytskyi, magharibi mwa Ukraine, alisema ulinzi wa anga uliangusha shabaha tisa za anga katika eneo lake.
Mamlaka za mitaa hazijapokea ripoti zozote za majeruhi au uharibifu wa mali, aliongeza.
Sio mara ya kwanza kwa Khmelnytskyi kulengwa - shambulio hili la kombora lilipiga eneo hilo mnamo Machi.
Sio mara ya kwanza kwa Khmelnytskyi kulengwa - shambulio hili la kombora lilipiga mkoa mnamo Machi
Wakati huo huo, gavana Vitaliy Kim alisema wanajeshi waliharibu ndege sita zisizo na rubani na makombora matatu ya cruise kwenye eneo la kusini la Mykolaiv.
Ukraine na Urusi mara nyingi hutuma ndege zisizo na rubani kuvuka mpaka lakini pande zote mbili zimesema zinalenga tu miundombinu ya kijeshi.