Umoja wa Ulaya wamuwekea vikwazo Waziri wa Ulinzi wa Iran na Walinzi wa Mapinduzi
EU imechapisha siku ya Ijumaa, Mei 31 katika Jarida Rasmi duru mpya ya vikwazo dhidi ya Iran, na haswa Pasdaran, Walinzi wa Mapinduzi. Kampuni tatu na watu sita wanalengwa.
Na mwandishi wetu mjini Brussels, Pierre Benazet
Hizi sio vikwazo vya kwanza vya Ulaya dhidi ya Iran, lakini mara hii walipiga drones na makombora ambayo Tehran inawapa washirika wake.
Katika orodha ya Wairani waliochukuliwa vikwazo na nchi za Umoja wa Ulaya wanaonekana kwanza Waziri wa Ulinzi, Mohammad Reza Gharaei Ashtiani, kisha mkuu wa Shirika la Viwanda vinavyotengeza vifaa vya anga na hatimaye Ismael Qaani, ambaye ni mkuu wa kikosi cha al-Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi, mrithi wa Qassem Soleimani, ambaye alifariki wakati wa shambulio la Marekani nchini Iraq.
Pia inakuja kampuni ya Kavan Electronics Behrad, na wakurugenzi wake wawili. Hii ni kampuni iliyobobea kwa kutengeneza vifaa na sehemu za ndege zisizo na rubani. Kisha makao makuu ya kampuni ya ujenzi ya Khatam al-Anbiya, kampuni ya uhandisi inayodhibitiwa na Walinzi, lakini pia Jenerali Gholam Ali Rashid, anayeiongoza kikos cha Walinzi wa Mapinduzi, Pasdaran. Hatimaye linakuja jeshi la wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi, kwa kuhusika kwake katika utoaji wa ndege zisizo na rubani na makombora kwa waasi wa Yemen, Houthi, na kwa Hezbollah ya Lebanon.
Vikwazo hivi kwa hakika vinagonga usafirishaji wote wa ndege zisizo na rubani na makombora yaliyokusudiwa washirika na maafisa wa Iran, kwani pamoja na Yemen na Hezbollah kuishambulia Israel, hii pia inahusu ndege zisizo na rubani zilizowasilishwa Urusi ili kushambulia Ukraine.