Utawala wa Kizayuni wakiri kushindwa katika kukabiliana na nguvu za kijeshi za muqawama wa Kiislamu wa Lebanon

 


  • Utawala wa Kizayuni wakiri kushindwa katika kukabiliana na nguvu za kijeshi za muqawama wa Kiislamu wa Lebanon.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimekiri kwamba nguvu za utawala huo za kuzuia mashambulio ya muqawama wa Kiislamu wa Lebanon katika eneo la kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) zimedhoofika na kutoweka kabisa.

Jumapili tarehe Pili Juni ulitimia mwezi wa nane wa mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza. Katika hali ambayo nchi za Kiarabu zimeshindwa kuchukua hatua yoyote ya kivitendo ya kusimamisha mauaji hayo ya kimbari, Hizbullah ya Lebanon na Yemen zimetangaza waziwazi kuwaunga mkono kijeshi watu wanaodhulumiwa wa Gaza. Jukumu la kukabiliana na Yemen limekabidhiwa muungano wa kijeshi wa Marekani na Uingereza, ambapo nchi mbili hizo zinaendesha mashambulio ya mara kwa mara dhidi ya watu wa Yemen. Sambamba na mauaji ya kimbari huko Gaza, utawala wa Kizayuni pia unafanya mashambulizi dhidi ya Hizbullah ya Lebanon, lakini hadi sasa umejiepusha kuingia katika makabiliano makubwa ya moja kwa moja na harakati hiyo ya muqawama.

Pamoja na hayo mashambulizi ya utawala wa Kizayuni hayajapelekea Hizbullah ya Lebanon kusimamisha harakati zake za kijeshi dhidi ya utawala huo ghasibu. Utawala wa Kizayuni haukuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu uwezo wa Hizbullah wa kuzuia mashambulizi ya adui na umekosoa katika mahesabu yake kuhusiana na harakati hiyo ya mapambano ya Kiislamu. Kuhusiana na suala hilo, vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimekiri kushindwa uwezo wa utawala huo kuzuia mashambulizi ya muqawama wa Kiislamu wa Lebanon na ukweli wa ahadi za Hizbullah, ambapo vinasema mwezi Mei uliopita ndio ulikuwa mwezi mgumu zaidi kwa Wazayuni katika mipaka ya kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) na Lebanon.

Askari wa Hizbullah

Sababu ya suala hili ni mapigo mazito na makali wanayoyapata kutoka kwa Hizbullah. Kwa mujibu wa shirika la habari la Israel "Walla", Hizbullah ya Lebanon imeshambulia maeneo ya kijeshi ya Israel na vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa makombora, na kuwasababishia Wazayuni hasara na maafa makubwa.

Katika miezi michache iliyopita, kufuatia jinai za kutisha za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na mauaji ya halaiki unayoyafanya dhidi ya Wapalestina wa ukanda huo, Hizbullah imelenga maeneo mengi ya kijeshi ya utawala huo kaskazini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, suala ambalo limeibua hofu kubwa miongoni mwa Wazayuni wanaoishi katika maeneo hayo. Mashambulizi hayo yanaonesha kuwa, Hizbullah iko tayari kukabiliana na utawala wa Kizayuni katika hali zote za kutokea vita vikubwa.

Nukta nyingine ambayo vyombo vya habari vya Kizayuni vimeitilia maanani ni uaminifu wa Hizbullah ya Lebanon. Huku utawala wa Kizayuni ukikanusha hasara na uharibifu unaosababishwa na mashambulizi ya Hizbullah, vyombo vya habari vya Kizayuni vinaamini kuwa Hizbullah inasema ukweli kuhusu suala hilo ambapo imeisababishia Israel pigo kubwa la kibinadamu na kimaada. Kuhusiana na hilo, tovuti ya habari ya Ahad imevinukuu vyombo vya habari vya Kizayuni na kuandika kuwa, adui Mzayuni amekuwa akificha idadi halisi ya majeruhi na hasara aliyopata katika medani ya vita ya Lebanon kwa takriban miezi minane iliyopita.

Hii ni katika hali ambayo muqawama wa Kiislamu wa Lebanon unasajili operesheni zake zote dhidi ya shabaha mbalimbali za adui na kuzirekodi kupitia Tume ya Taarifa za Vita. Tovuti hiyo ya habari imeongeza kuwa, matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na vyombo vya habari vya Kizayuni kuhusu uaminifu wa Hizbullah na Tel Aviv yanaonyesha kuwa, asilimia 80 ya Wazayuni wanaichukulia Hizbullah kuwa aminifu zaidi katika masuala yanayohusiana na habari na vitisho inavyotoa.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China