Vikosi vya Yemen vyatumia kombora jipya la balistiki dhidi ya Israel

 

  • Vikosi vya Yemen vyatumia kombora jipya la balistiki dhidi ya Israel

Vikosi vya Wanajeshi vya Yemen vimetangaza kutumia kombora jipya la balistiki dhidi ya shabaha ya eneo la kijeshi la utawala haramu wa Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu katika operesheni mpya ya kuiunga mkono Palestina.

Msemaji wa vikosi hivyo Brigedia Jenerali Yahya Saree alitoa tangazo hilo siku ya Jumatatu. Amesema kombora hilo jipya la balistiki lililotumiwa limepewa jina la "Palestina," na lilivurumishwa katika ngome ya kijeshi ya Israel katika mji wa Um al-Rashrash, ambao pia unajulikana kama Eilat.

Jenerali Saree amesema Kombora hilo "limetumika kwa mara ya kwanza," na ameongeza kuwa operesheni hiyo ilitekelezwa kwa mafanikio.

Vikosi vya Yemen vimetekeleza operesheni nyingi za kuunga mkono Wapalestina tangu Oktoba mwaka jana, wakati utawala wa Israel ulipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Zaidi ya Wapalestina 36,470, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wameuawa katika vita hivyo vilivyoanza kufuatia operesheni ya kulipiza kisasi iliyofanywa na harakati za kupigania ukombozi wa Palestina huko Gaza.

Kombora la Jeshi la Yemen likitayarishwa

Mbali na kulenga ngome za jeshi la Israel ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo, wanajeshi wa Yemen wamekuwa wakilenga meli za Israel au zile zinazoelekea kwenye bandari za utawala huo.

Jenerali Saree amesisitiza kuwa "Vikosi vya Wanajeshi vitaendelea na operesheni za kijeshi kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Gaza na kwa mshikamano na watu wanaodhulumiwa wa Palestina."

Amesema operesheni hizo zitadumu kwa muda mrefu kama utawala wa Israel utaendelea na vita na mzingiro ambao umekuwa ukitekeleza kwa wakati mmoja dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China