Waathiriwa wa msukosuko uliotokea katika shirika la ndege la Singapore kufidiwa

 .

Shirika la ndege la Singapore limejitolea kuwalipa fidia wale waliojeruhiwa kwenye safari ya ndege ya London kwenda Singapore iliyokumbana na misukosuko mikali.

Shirika hilo la ndege lilisema linajitolea kuwalipa $10,000 (£7,800) wale waliopata majeraha madogo, katika chapisho la Facebook.

Kwa abiria walio na majeraha mabaya zaidi, shirika la ndege linatoa "malipo ya mapema ya $25,000 kushughulikia mahitaji yao ya haraka" na majadiliano zaidi ili kukidhi "hali zao".

Abiria wa Uingereza mwenye umri wa miaka 73 alifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati ndege ya SQ 321 ilipokumbana na misukosuko nchini Myanmar na kuelekezwa Thailand mwezi Mei.

Shirika la ndege la Singapore bado halijajibu ombi la BBC kuhusu ni watu wangapi wanastahili malipo hayo.

Zaidi ya watu mia moja waliokuwa kwenye SQ 321 walitibiwa katika hospitali ya Bangkok kufuatia ya tukio hilo.

Uchunguzi wa mapema ulionyesha kuwa ndege hiyo iliongeza kasi ya juu na chini, na kushuka karibu 178ft (54m) kwa zaidi ya sekunde 4.6.

Abiria walielezea jinsi wafanyakazi na wale ambao hawakufunga mikanda walivyolazimika kuruka na kugonga dari ya ndege hiyo.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Hamas yadai kuwakamata wanajeshi wa Israel lakini Israel imekanusha madai hayo