Waziri wa vita wa Israel Benny Gantz ajiuzulu katika serikali ya dharura

 

Waziri wa vita katika baraza la dharura nchini Israel Benny Gantz amejiondoa serikalini katika ishara ya kuzidisha mgawanyiko kuhusu mipango ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu baada ya mzozo kuhusu Gaza.

Akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari mjini Tel Aviv Jumapili ambapo alitangaza kujiuzulu, Bw Gantz alisema uamuzi huo ulifanywa kwa "moyo mzito".

"Kwa bahati mbaya, Bw Netanyahu anatuzuia kukaribia ushindi wa kweli, ambao ni uhalali wa mzozo unaoendelea," alisema.

Akichukuliwa na baadhi ya watu kuwa mgombea anayeweza kuwania mamlaka nchini Israel, Bw Gantz alitoa wito kwa Bw Netanyahu kupanga tarehe ya uchaguzi.

Waziri wa vita katika baraza la dharura nchini Israel Benny Gantz

Bw Netanyahu alijibu kwa chapisho kwenye X: "Benny, huu sio wakati wa kuacha kampeni, huu ni wakati wa kuungana." Kiongozi wa upinzani Yair Lapid aliunga mkono uamuzi wa Bw Gantz kama "muhimu na sahihi" kwenye mitandao ya kijamii.

Mara tu baada ya tangazo hilo, Waziri wa mrengo wa kulia wa Usalama wa Kitaifa Itamar Ben-Gvir aliomba kupewa nafasi hiyo ya waziri wa vita katika baraza la mawaziri la dharura.

Bw Ben-Gvir ni sehemu ya muungano wa mrengo wa kulia ambao umetishia kujiondoa na kuiangusha serikali ikiwa Israel itakubali pendekezo la kusitisha mapigano lililotolewa na Rais wa Marekani Joe Biden.

Mwezi uliopita, Bw Gantz aliweka makataa ya Juni 8 kwa Bw Netanyahu kuweka bayana jinsi Israel itaafikia "malengo yake ya kimkakati" sita, ikiwa ni pamoja na kumalizika kwa utawala wa Hamas huko Gaza na kuanzishwa kwa utawala wa kiraia wa kimataifa katika eneo hilo.

Waziri Mkuu alitupilia mbali maoni hayo wakati huo na kusema "maneno yasiyo na msingi" ambayo yangemaanisha "kushindwa kwa Israeli".

Jenerali mstaafu wa jeshi na mkosoaji wa mara kwa mara wa Bw Netayanhu,

Bw Gantz alikuwa mjumbe wa "baraza la mawaziri la vita" la Israel linalofanya maamuzi, pamoja na waziri mkuu na Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China