Umuhimu na taathira za wimbi jipya la operesheni za vikosi vya Yemeni katika Bahari Nyekundu dhidi ya vikosi vya Marekani


  • Umuhimu na taathira za wimbi jipya la operesheni za vikosi vya Yemeni katika Bahari Nyekundu dhidi ya vikosi vya Marekani

Vikosi vya Yemen vimefanikiwa kutekeleza oparesheni mpya kadhaa dhidi ya meli zinazosindikizwa na manowari za Marekani katika Bahari Nyekundu na ya Mediterania.

Yahya Saree, Msemaji wa Jeshi la Yemen ametangaza katika taarifa kuwa vikosi vya majini, ndege zisizo na rubani na makombora vya jeshi la Yemen vimefanikiwa kutekeleza operesheni 6 za kijeshi dhidi ya meli 6 katika Bahari ya Mediterania na Bahari Nyekundu (Bahari ya Sham).

Akiashiria kwamba mashambulio dhidi ya meli hizo yote yamefanywa kutokana na meli hizo kukiuka sheria inayopiga marufuku meli kuingia katika bandari za Palestina inayokaliwa kwa mabavu, Yahya Saree amesisitiza kwamba operesheni hizo kubwa za jeshi la Yemen zimefanyika kwa ajili ya kulisaidia taifa linalodhulumiwa la Palestina na kukabiliana na jinai za adui Mzayuni dhidi ya wakimbizi wa Kipalestina katika eneo la Rafah.

Saree amesema: Meli ya "LAAX" katika Bahari Nyekundu pamoja na meli za "MOREA" na "Sealady" zimelengwa kwa makombora ya balistiki ya vikosi vya Yemeni na mashambulio ya ndege zisizo na rubani. Msemaji wa jeshi la Yemen ameongeza kuwa meli za Marekani za "ALBA", "Maersk HARTFORD" na "MINERVA ANTONIA" zimelengwa katika Bahari ya Mediterania kwa makombora kadhaa ya cruise.

Moja ya operesheni za vikosi vya Yemeni kwenye Bahari Nyekundu 

Shirika la kigaidi la "CENTCOM" pia limeripoti kuwa vikosi vya Yemen vimerusha makombora matano ya balestiki kuelekea Bahari Nyekundu (Sham). Hata kama viongozi wa Marekani wanadai kuwa meli hizo zinamilikiwa na nchi tofauti na kuwa zinabebea mizigo tofauti ya kibiasha lakini ukweli wa mambo ni kwamba hapana shaka kuwa meli hizo hubeba bidhaa mbalimbali na mara nyingi silaha, ambazo baada ya kupakuliwa katika bandari za ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) hatimaye huishia mikononi mwa utawala wa Kizayuni.

Serikali za Marekani na nchi nyingine za Magharibi hutumia meli hizo kupeleka kila aina ya vifaa kwenye ardhi zionazokaliwa kwa mabavu (Israel) kwa kisingizio cha kusafirisha bidhaa za kibiashara. Mwenendo huo umepanuka katika miezi ya hivi karibuni kufuatia kushindwa mfululizo kwa jeshi la Kizayuni katika kukabiliana na vikosi vya muqawama, ambapo Marekani na serikali za Magharibi zinatumia njia ya Bahari Nyekundu kutuma bidhaa na hasa silaha kwa ajili ya kuusaidia utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita na ikiwa ni katika kuwaunga mkono watu wa Gaza, jeshi la Yemen limelenga meli kadhaa za utawala wa Kizayuni au meli zinazobeba mizigo kwa ajili ya utawala huo, ambazo zilikuwa zinaelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, katika Bahari ya Shamu, Bahari ya Hindi na Lango Bahari la Bab al-Mandab. Operesheni hizo kubwa za jeshi la Yemen mbali na kukwamisha juhudi za Marekani na Uingereza za kuvunja mzingiro wa majini dhidi ya utawala wa Kizayuni, zimethibitisha nguvu za jeshi la Yemen ambazo Washington haikuwa na habari nazo na hivyo kuwashangaza Wamarekani.

Vikosi vya jeshi la Yemen vimeahidi kuendelea kuzishambulia meli za utawala huo au zinazoelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu pamoja na meli za jeshi la muungano unaounga mkono utawala wa Kizayuni katika Bahari Nyekundu hadi pale utawala huo haramu utakapoamua kusimamisha mashambulizi na mauaji yake ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Gaza. Bahari ya Sham ina nafasi muhimu katika usafiri wa baharini na ni ghuba katika Bahari ya Hindi ambayo iko kati ya Bara Arabu na kaskazini mashariki mwa bara la Afrika. Lango la Bab al-Mandab linaunganisha Bahari ya Hindi na Mfereji wa Suez unaoungana na Bahari ya Mediterania upande wa kaskazini. Bahari ya Sham ndio mpaka kati ya mabara mawili ya Asia na Afrika.

Wimbi jipya la mashambulizi na operesheni za vikosi vya Yemen linaonyesha uwezo wa vikosi vya kieneo katika kukabiliana na uingiliaji wa kigeni na athari zake hasi katika eneo. Jeshi la Marekani licha ya kuwa na suhula zote na uwekezaji mkubwa wa kifedha na zana za kisasa, lakini halijaweza kusimamisha operesheni za jeshi la Yemen na hivyo kuanika peupe udhaifu wao katika uwanja huo.

Operesheni ya jeshi la Yemen ni sehemu ya majibu madhubuti na makali ya vikosi vya muqawama vya Iraq, Lebanon na makundi ya wapiganaji wa ukombozi wa Palestina, ambayo yalianza miezi michache iliyopita kufuatia operesheni ya "Kimbunga cha Al-Aqsa" dhidi ya uvamizi na jinai za Wazayuni, na yanaendelea kupata mafanikio makubwa katika nyanja tofauti za kimkakati na kimbinu.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China