Ukraine yaendelea kusonga mbele ndani ya eneo la Urusi

 

Ukraine yaendelea kusonga mbele ndani ya eneo la Urusi

.

Chanzo cha picha, Reuters

Eneo la mpaka wa magharibi mwa Urusi la Kursk lilikumbwa na shambulio la kushtukiza wiki iliyopita, na kusababisha mamlaka ya Urusi kutangaza hali ya hatari katika eneo hilo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema wanajeshi wamesonga mbele kilomita 1-2 zaidi ndani ya eneo la Kursk tangu Jumatano asubuhi, na pia wamewakamata wanajeshi 100 wa Urusi.

Lakini Urusi inadai kuwa imefanikiwa kusitisha hatua za Ukraine za kusonga mbele zaidi.

Sasa katika wiki yake ya pili, huu ni uvamizi mkubwa zaidi wa Ukraine ndani ya Urusi tangu Moscow ilipoanzisha uvamizi wake mnamo mwaka 2022.

Kiasi cha eneo la Urusi lililonyakuliwa hakijulikani, huku nchi zote mbili zikitoa kauli zinazokinzana.

Kamanda wa kitengo cha kikosi maalum cha Chechen Akhmat, Meja Jenerali Apti Alaudinov aliwaambia watazamaji kwenye Televisheni inayodhibitiwa na serikali ya Urusi, Channel One, kwamba vikosi vya Urusi viko karibu "kuwazuia" wanajeshi wa Ukraine kuendelea kusonga mbele.

Lakini katika video moja, mkuu wa jeshi Oleksandr Syrskyi alisema wanajeshi wa Ukraine sasa wanadhibiti kikamilifu mji wa mpakani wa Kursk wa Sudzha.

Hata hivyo, BBC haikuweza kuthibitisha dai hili kwa uhuru, lakini ripoti ya televisheni ya Ukraine iliyorekodiwa kutoka ndani ya mji ilionyesha wanajeshi wa Ukraine wakiondoa bendera ya Urusi kutoka kwenye shuleni moja.

Huku kukiwa na madai ya Ukraine kupata mafanikio ya kudhibiti maeneo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ukraine Heorhiy Tykhy alisema hawana nia ya "kuchukua" eneo la Urusi. "

Urusi ikikubali kurejesha amani ya haki haraka iwezekanavyo... ndivyo uvamizi wa vikosi vya ulinzi vya Ukraine nchini Urusi utakavyofikia tamati," aliwaambia waandishi wa habari.

Katika mkutano wa awali na maafisa wa serikali, Bw Zelensky alisema atafikiria kuanzisha "ofisi za makamanda wa kijeshi" katika eneo hilo.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China