US: Yumkini Iran na Muqawama zikafanya 'mashambulio makubwa' dhidi ya Israel wiki hii
US: Yumkini Iran na Muqawama zikafanya 'mashambulio makubwa' dhidi ya Israel wiki hii
Marekani imeonya kuwa Iran na Harakati za Muqawama katika eneo zinaweza kufanya "mashambulizi makubwa" dhidi ya utawala wa Israel ya kulipiza kisasi cha mauaji yaliyofanywa mwezi uliopita ya kiongozi wa Hamas Ismail Haniya.
Utawala wa Kizayuni umekuwa ukijipapatua na kukanusha kuhusika na ukatili huo, lakini Jamhuri ya Kiislamu imesisitiza kuwa Tel Aviv inawajibika kikamilifu na imeapa kuwa itatoa jibu kali.
Siku ya Jumatatu, Brigedia Jenerali Ali Shadmani, Naibu Mratibu wa Idara ya Khatamul-Anbiya ya Makao Makuu ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) alisisitiza kuwa, ulipizaji kisasi kwa Jamhuri ya Kiislamu kwa utawala wa Kizayuni "uko njiani."
Mauaji ya kigaidi ya Shahidi Ismail Haniya yalifanywa siku moja tu baada ya shambulio la anga la Israel dhidi ya mji mkuu wa Lebanon Beirut yaliyopelekea kuuawa shahidi Fuad Shukr, kamanda mkuu wa Hizbullah na mshauri wa Katibu Mkuu wa harakati hiyo ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Sayyed Hassan Nasrullah.
Hizbullah kwa upande wake, nayo pia imeahidi kutoa jibu kali kwa utawala haramu wa Israel la ulipizaji kisasi.
Harakati za Muqawama za Iraq na Yemen nazo pia zimeapa kuwa zitaungana na Iran na Hizbullah katika kulipiza kisasi cha damu ya Shahidi Ismail Haniya na Shahidi Fuad Shukr.../