Wazayuni wazidi kujawa na hofu na kiwewe cha kungojea ulipizaji kisasi wa Mhimili wa Muqawama
Wazayuni wazidi kujawa na hofu na kiwewe cha kungojea ulipizaji kisasi wa Mhimili wa Muqawama
Aug 12, 2024 11:05 UTC
Utawala wa Kizayuni wa Israel umerefusha muda wa kuviweka katika hali ya tahadhari vikosi vya jeshi lake la anga kwa kuhofia madhara makubwa yatakayosababishwa na jibu la ulipizaji kisasi la Mhimil wa Muqawama kufuatia mauaji ya Ismail Haniya, aliyeuliwa shahidi na utawala huo wa kigaidi.
Shahidi Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati
ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS na mmoja wa walinzi wake
waliuawa shahidi tarehe 31 Julai kutokana na hujuma ya kigaidi
iliyofanywa mjini Tehran.
Wasiwasi na mkanganyiko wa kiakili unaousokota utawala haramu wa
Israel unazidi kuongezeka siku baada ya siku kwa kuhofia ukubwa wa jibu
lisilo na shaka la Iran kwa mauaji ya Shahidi Ismail Haniya na la
Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon kutokana na kuuliwa kamanda wake mkuu
Shahidi Fuad Shukr.
Kwa mujibu wa IRNA, tovuti ya Walla ya utawala wa Kizayuni imeeleza
kuhusiana na hilo kwamba kiwango cha hali ya hadhari ya intelijesnia
ya kijeshi na jeshi la anga la Israel kimeongezwa kwa kuzingatia
makadirio ya ukubwa wa jibu linalokaribia kutolewa na Iran.
Redio ya utawala wa Kizayuni imeashiria barabara zilivyobaki tupu na wasiwasi uliotanda kwenye uso wa kila Mzayuni na kuielezea hali hiyo kuwa ni sawa na ilivyokuwa wakati wa kipindi cha Corona.
Wasiwasi na hofu hiyo haijawapata wakazi pekee wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, bali imewakumba pia viongozi wa Kizayuni.
Yoav Gallant, waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni amesema katika
mazungumzo yake na waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin kuhusu jibu
la kulipiza kisasi la Iran kwa utawala huo ya kwamba: Iran inajiandaa
kwa mashambulizi makubwa dhidi ya Israel; na makadirio ya shirika la
ujasusi la Israel zinaonyesha kuwa, mashambulizi ya kulipiza kisasi ya
Iran kutokana na mauaji ya Haniya yatafanyika katika siku zijazo.
Kwa vile utawala wa Kizayuni hauwezi peke yake kuyahimili
mashambulizi ya Tehran, viongozi wa utawala huo wanahitaji msaada wa
Marekani kwa ajili ya kujilinda, sawa na ilivyokuwa katika shambulio la
Iran la Aprili 14.../