Duru za Hezbollah zinasema Nasrallah yuko salama kufuatia mashambulizi ya anga ya Israel

 Duru za Hezbollah zinasema Nasrallah yuko salama kufuatia mashambulizi ya anga ya Israel


Vyanzo vya usalama vya Hezbollah vimeiarifu Press TV kwamba Sayyed Hassan Nasrallah, kiongozi wa harakati ya muqawama, yuko katika eneo salama na hajadhurika na mashambulizi ya hivi karibuni ya anga ya Israel katika viunga vya kusini mwa Beirut.

Kauli hii inafuatia uvumi ulioenea kwenye mitandao ya kijamii unaodai kuwa Nasrallah alilengwa wakati wa shambulio kubwa la anga la utawala wa Israel kwenye kitongoji cha Dahiya kusini mwa Beirut siku ya Ijumaa.

Ripoti pia zilisema Sayyed Hashem Safieddine, mkuu wa Halmashauri Kuu ya Hezbollah yuko salama, huku shirika la habari la Iran la Tasnim likinukuu vyanzo vya habari nchini Lebanon kuwa hakuna kamanda wa Hezbollah aliyeuawa shahidi katika mashambulizi ya kigaidi ya Israel.

Majengo sita yalibomolewa chini kutokana na uvamizi wa Israel kwenye kitongoji cha kusini cha Beirut.

Wizara ya Afya ya Lebanon imesema takriban watu wawili wameuawa shahidi na wengine 76 kujeruhiwa katika shambulio hilo.

Redio ya jeshi la Israel ilisema kuwa ndege ya F-35 ilifanya uchokozi huo kwa kutumia mabomu ya bunker-buster.

Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa utawala huo uliitaarifu Marekani kuhusu shambulio hilo muda mfupi kabla ya kutekelezwa.

Vyombo vya habari vya Lebanon vilisema wanajeshi wa ulinzi wa raia walikuwa wanafanya kazi ya kuzima moto uliozuka katika eneo hilo na kuwaondoa waliojeruhiwa.

Waziri Mkuu wa muda wa Lebanon Najib Mikati alijibu shambulio hilo, akisema jumuiya ya kimataifa inapaswa kumzuia adui wa Israel na kuacha dhuluma yake na vita vya maangamizi vinavyoendelea dhidi ya Lebanon.

Mikati alisema shambulio la Israel linaonyesha kutopendezwa kwa utawala huo na miito ya kimataifa ya kusitisha mapigano.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China