Israel yashambulia mji wa kihistoria wa Baalbek nchini Lebanon

 

Israel yashambulia mji wa kihistoria wa Baalbek nchini Lebanon

Moshi

Chanzo cha picha, AFP

Mashambulizi ya Israel yamesababisha watu 19 kupoteza maisha, wakiwemo wanawake wanane, karibu na mji wa Baalbek mashariki mwa Lebanon, wizara ya afya ya nchi hiyo imesema.

Hilo limejiri saa chache baada ya makumi ya maelfu ya wakazi kukimbia kutokana na maagizo ya kuwahamisha yaliyotolewa na jeshi la Israel.

Meya Mustafa al-Shell aliiambia BBC zaidi ya mashambulizi 20 yaliripotiwa Jumatano alasiri katika eneo la Baalbek, na matano ndani ya jiji lenyewe, ambapo kuna jumba la hekalu la kale la Kirumi lililotambuliwa na Unesco.

Jeshi la Israel lilisema kuwa limeshambulia vituo vya amri na udhibiti vya Hezbollah na miundombinu huko Baalbek na Nabatiyeh, kusini mwa Lebanon.

Jeshi pia lilisema lililenga vituo vya mafuta vya Hezbollah katika Bonde la Bekaa, ambako Baalbek ipo.

Halikutoa maelezo yoyote, lakini shirika la habari la serikali ya Lebanon lilisema matangi ya dizeli yalipigwa katika mji wa Douris, ambapo Bw Shell alisema picha zilionesha moshi mwingi mweusi ukipanda angani.

Mashambulizi hayo yamekuja huku katibu mkuu mpya wa Hezbollah akisema kundi hilo litaendeleza mpango wake wa vita dhidi ya Israel chini ya uongozi wake na kwamba "halitadai" kusitishwa kwa mapigano.

Akizungumza siku moja baada ya uteuzi wake kutangazwa, Naim Qassem alisema atafuata ajenda ya mtangulizi wake, Hassan Nasrallah, ambaye aliuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel mjini Beirut mwezi uliopita.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China