Jaribio la Gachagua kuzuia kuapishwa kwa Kindiki lagonga mwamba

 

Jaribio la Gachagua kuzuia kuapishwa kwa Kindiki lagonga mwamba

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mahakama Kuu nchini Kenya imeondoa amri zinazomzuia Naibu Rais Mteule Kithure Kindiki kuapishwa.

Wakati wakitoa uamuzi huo, jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Eric Ogola, Anthony Mrima na Fredah Mugambi walisema kuwa afisi ya kikatiba ya naibu rais haiwezi kuachwa wazi.

David Munyi Mathenge na Peter Gichobi Kamotho walitaka mahakama kuweka maagizo ya kusitisha kuapishwa kwa Kindiki Kithure kama Naibu Rais mpya baada ya Bunge la Kitaifa kuidhinisha uteuzi wake, siku moja baada ya Bunge la Seneti kupiga kura ya kumtimua Rigathi Gachagua.

David Munyi Mathenge na Peter Gichobi Kamotho walitaja suala hilo kuwa la "umuhimu mkubwa na udharura wa kitaifa."

Wakitoa uamuzi wao, jopo la majaji watatu waliendelea kusema kwamba kesi hiyo itatajwa Novemba 7, 2024, na kuongeza kuwa Gachagua yuko huru kuwasilisha rufaa dhidi ya uamuzi huo.

"Maombi ya maagizo yakumzuia Naibu Rais Mteule Kithure Kindiki kuapishwa yamekataliwa. Maagizo hayo yaliyotolewa mnamo Oktoba 18, 2024 katika Mahakama Kuu ya Kerugoya yanaondolewa na/au kuwekwa kando. Kuna uhuru wa kukata rufaa. Nakala za maelezo ya kesi hii yaliyochapishwa na nakala zilizoidhinishwa za uamuzi huu zitatolewa kwa wahusika kwa gharama. Tutaitaja kesi hii mnamo Novemba 7, 2024 saa nane mchana katika mahakama ya wazi,” majaji walisema kwenye uamuzi huo uliosomwa na Jaji Ogola.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China