Korea Kaskazini yarusha kombora linaloshukiwa kuwa la masafa marefu

 

Korea Kaskazini yarusha kombora linaloshukiwa kuwa la masafa marefu

Kombora

Chanzo cha picha, Reuters

Korea Kaskazini imerusha kombora linalodaiwa kuwa la masafa marefu (ICBM) kuelekea baharini katika pwani yake ya mashariki, jeshi la Korea Kusini lilisema.

Tukio hilo linakuja wakati uhusiano kati ya Korea mbili hizo mbili unavyozidi kuwa mbaya.

Kombora hilo lilirushwa mwendo wa takribani saa 07:10 za huko siku ya Alhamisi (22:10 GMT Jumatano).

Korea Kusini ilikuwa imeonya Jumatano kwamba Kaskazini ilikuwa inajiandaa kuirusha ICBM yake wakati wa uchaguzi wa urais nchini Marekani tarehe 5 Novemba.

Mara ya mwisho Korea Kaskazini ilirusha kombora la ICBM mwezi Disemba mwaka jana, kinyume na vikwazo vya muda mrefu na vile vile vya Umoja wa Mataifa.

Nchi jirani ya Japan ilisema kuwa ilifuatilia urushaji wa kombora wa Alhamisi, na kuongeza kuwa kombora hilo lilitarajiwa kuanguka baharini ifikapo 08:40 saa za huko.

Tukio hilo la Alhamisi linakuja baada ya Korea Kusini na Marekani kuishutumu Korea Kaskazini kwa kutuma wanajeshi wake nchini Urusi kusaidia vita vya Vladimir Putin nchini Ukraine.

Kudaiwa kuwepo kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi kumeongeza wasiwasi kuhusu kuimarika kwa uhusiano kati ya Putin na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China