Mahakama ya rufaa yakataa ombi la Gachagua la kusitisha Mahakama Kuu kusikiliza kesi yake
Mahakama ya rufaa yakataa ombi la Gachagua la kusitisha Mahakama Kuu kusikiliza kesi yake
Naibu Rais aliyeondolewa madarakani Rigathi Gachagua amepata pigo lingine baada ya mahakama ya rufaa kukataa kutoa maagizo ya kusimamisha Mahakama Kuu kuendelea kusikiliza kesi yake ya kuondolewa madarakani.
Gachagua alikwenda mahakama ya rufaa akisema kuwa hajaridhishwa na uamuzi uliotolewa wiki jana na jopo la majaji watatu iliyoidhinisha uamuzi wa Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu wa kuunda jopo la majaji hao kusikiliza kesi za Gachagua.
Rigathi Gachagua alikuwa amesema Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu hana mamlaka ya kuunda jopo hilo, isipokuwa jopo kama hilo linaweza kuundwa tu na Jaji Mkuu.
Hatima ya Gachagua sasa iko kwa Mahakama Kuu ambayo kwa sasa inaendelea kutoa uamuzi juu ya kesi ya kuzuia kuapishwa kwa Naibu Rais mteule Kithure Kindiki.
Jopo la majaji hao ni pamoja na Jaji Anthony Mrima, Eric Ogola na Fredah Mugambi.