'Mimi sio mpiga kura wa suala moja, lakini hili ni kubwa': Utoaji mimba uliamua kura za wanawake hawa

 

'Mimi sio mpiga kura wa suala moja, lakini hili ni kubwa': Utoaji mimba uliamua kura za wanawake hawa

Graphic with the faces of four women voters
  • Author, Rachel Looker
  • Nafasi, BBC News, Washington

Uchaguzi wa urais wa 2024 ni wa kwanza tangu Mahakama ya Juu ilipobatilisha uamuzi wa Roe v Wade, ambao ulilinda haki ya kitaifa ya kutoa mimba.

Mgawanyiko wa kijinsia umekuwa mkubwa katika uchaguzi huu, huku kura za maoni zikionyesha Kamala Harris ana uongozi miongoni mwa wanawake na Rais wa zamani Donald Trump anaongoza kwa upande wa wanaume.

BBC imekuwa ikizungumza na wapiga kura wanawake kuhusu jinsi wanavyozingatia jinsia na uavyaji mimba huku wakipiga kura katika siku za mwisho za kampeni.

Graphic with photo of Michelle Allen, 38, of Arizona

Michelle anafanya kazi kama mhandisi wa ubora huko Arizona. Ana umri wa miaka 38 na ni mwanachama wa chana cha Republican , lakini anapanga kumpigia kura Kamala Harris.

Nina wasiwasi kuhusu haki za wanawake na afya ya wanawake. Mimi si mpiga kura wa suala moja, lakini hilo ni kubwa sana. Ninafanya kazi katika sekta ya matibabu na niliathiriwa sana kibinafsi na kupinduliwa kwauamuzi wa Roe v Wade kwa sababu sikuweza kupata dawa nyingi nilizohitaji. Hakuna mtu aliyekuwa na uhakika na uhalali uliokuwepo... ingawa hutumiwa kwa mambo mengine.

Msimamo mzima wa Republican ni serikali ndogo na usiruhusu serikali kufanya maamuzi yangu ya kibinafsi, kwa nini wanajaribu kutunga sheria ambayo itaamua mwanamke anaweza kufanya kipi na mwili wake?

[Urais wa Harris]utamaanisha kwamba mambo yote ambayo wazazi wangu waliniambia nilipokuwa mdogo yalikuwa ya kweli - kwamba kwa sababu tu wewe ni msichana haimaanishi kwamba una mipaka.

Graphic with photo of Tracey Sorrell, 53, of Texas

Muuguzi huyu kutoka Texas alimpigia kura Trump wakati wa uchaguzi uliopita wa urais na anapanga kumuunga mkono tena.

[Trump] bila shaka amesema mambo ambayo pengine hangepaswa kuyasema. Nitalazimika kutikisa kidole kwa hilo, haswa kama mwanamke, lakini bado sijasikia chochote ambacho kingenifanya nibadilishe mawazo yangu kuhusu kura yangu.

Mimi sipigii kura sifa za mtu. Ninapia kura kwa ajili ya sera zake . Si lazima niolewe na huyo mwanaume. Sihitaji kushughulika naye. Lazima nishughulike na sera zake.

Wakati wa kutoa mimba, [Harris] hatoi vigezo vya ujauzito utadumu muda gani kabla ya mtu kuruhusiwa kutia mimba.

Hiyo haiwezi kuacha kuwa wazi. Nilikuwa NICU [kitengo cha wagonjwa mahututi ambao ni watoto wachanga] kwa miaka 17... Ninajali haki za wanawake. Ninajali wanawake. Mama ndiye mgonjwa wa kwanza. Walakini, sijavutiwa kwamba hatatoa jibu kwa hilo.


Graphic with photo of Feana Nevel, 38, of Illinois

Mwanachama huyu wa chama cha Democratic kutoka Illinois anapanga kumpigia kura Harris siku ya uchaguzi. Hapo awali aliunga mkono tikiti ya Democratic mnamo 2020, akimpigia kura Joe Biden.

Hakika nina wasiwasi kuhusu mwelekeo ambao haki za uzazi zinaendelea katika sehemu fulani za nchi. Ninahisi kwamba majaribio ya Trump ya kusema kwamba anaelewa ni kwa nini [haki za uzazi] ni suala muhimu kwa wanawake yamefeli kwa kiasi kikubwa.

Nadhani Harris ana ufahamu wa ndani wa umuhimu wake, kwa sababu sio tu mwanamke lakini pia mwanamke mwenye asili ya watu weusi/waafrika. Je, ningependa aweke mipango yake zaidi kidogo ili uwezekano wa kupanua haki za uzazi? Ndiyo. Lakini Trump ameweka kizuizi cha chini sana kwamba angeweza kuendelea hata kutaja na bado angekuwa anafanya kazi nzuri zaidi.

[Urais wa Harris] hunitoa machozi nikifikiria kuhusu uwezekano huo. Nina binti wa miaka tisa na ana umri wa kutosha kuanza kuwa na matamanio na kuanza kutilia maanani ulimwengu unaomzunguka.

Graphic with photo of Karen Comeau, 63, of Illinois

Msaidizi huyu wa maktaba alimpigia kura Trump mnamo 2020, lakini sasa bado hajaamua na anafikiria "kumwandikia" mgombeaji - kumpigia kura mtu ambaye hagombei rasmi.

Hii sio mara yangu ya kwanza na nimefika hatua katika maisha yangu ambapo ninaweza kutazama nyuma matangazo wanaofanyi vikundi viwili maalum.

Inashangaza kwamba tuna Harris kama mwanamke anayegombea urais kwa dhati na kwamba amekuwa makamu wa rais na ana uzoefu fulani. Lakini Trump, alipokuwa ofisini, sikuchukizwa sana na alichokuwa akifanya.

Sitajali kuwa na rais mwanamke lakini baadhi ya misimamo ya kisiasa ya Harris na kile ninachofikiri ni sawa haviendani.

Graphic with photo of Angela Richardson, 27, of Iowa

Angela ni mwanafunzi aliyehitimu huko Iowa. Akiwa mwanachama wa Democrat, alimuunga mkono Biden katika uchaguzi uliopita wa rais na anapanga kumpigia kura Harris.

Ningependa sana huu uwe wakati wa kusherehekea tunapomchagua mwanamke wa kwanza mwenye asili ya mtu mweusi kwenye ofisi yetu ya juu zaidi, lakini kwa bahati mbaya jinsi uchaguzi ulivyo mgumu dhidi ya Trump na jinsi kambi ya kampeni ya [Harris] imekuwa ya kukatisha tamaa katika baadhi ya masuala muhimu kwangu , imekuwa vigumu kuwa na sherehe kama ningevyotamani.

Ni wazi kwamba uavyaji mimba ni suala kubwa linalohitaji kushughulikiwa, lakini si lazima nifurahie mbinu za mgombea yeyote katika kushughulikia suala hilo.

Ninaelewa kuwa Harris ana sera ambapo anataka kuratibu Roe v Wade, lakini nadhani haki na masuala ya wanawake yanaenea nje ya ufikiaji wa uavyaji mimba. Trump ni mwoga sana katika suala la haki za wanawake, kwa hivyo ni vigumu kumweka chini kwa msimamo wowote.

Graphic with photo of Ursula Duebel, 72, of California

Mwana Republican huyu mstaafu ambaye anapanga kumpigia kura Trump. Pia alimuunga mkono rais huyo wa zamani mnamo 2020.

Nadhani [Trump] ndiye pekee anayewezekana kwa sababu nadhani Harris hana maarifa na hana uwezo. Nadhani atakuwa janga kwa nchi hii, nikisikiliza maneno yake akikwepa kuzungumzia mambo muhimu . Ninapata tu hisia za kutisha juu yake.

Graphic with photo of Abigail Burke, 38, of Florida

Mpiga kura huyu huru alimpigia kura Biden katika uchaguzi wa urais wa 2020 na alipiga kura kwa barua mwaka huu akimuunga mkono Harris.

Haki za uzazi kwa wanawake ni kubwa kwangu kama mwanamke, haswa ninayeishi katika jimbo la Florida ambapo kuna marekebisho kwenye kura ambayo yatahakikisha ulinzi wa haki za uavyaji mimba.

Natamani sana kuunga mkono chama kitakachounga mkono haki ya uzazi kwa wanawake na sio wanawake tu, bali kwa kila mtu, kwani ni nini cha kusema kuwa hakitaenea mahali pengine? Inaanza na wanawake, kwa kawaida, lakini inaendelea na kuendelea.

Serikali yetu iko nyuma kwa angalau miaka 50 kwa mambo mengi - haswa nchi zingine ulimwenguni zenye uwakilishi bora. Nina mpwa wangu ambaye ninampenda sana. Ukweli kwamba anaweza kumuona [rais mwanamke], na ili tu hilo liwe jambo la kawaida kwake, litakuwa kubwa.

Graphic with photo of Catherine Estes, 49, of Georgia

Mpiga kura huyu huru kutoka Georgia anajielezea kama mtu mwenye msimamo wa wastani anayeegemea mrengo wa kushoto. Kwa sababu ya imani yake na maoni yake dhidi ya uavyaji mimba, haungi mkono Harris au Trump mwaka huu.

Kwa kweli nilikuwa naenda kumpigia kura Harris, lakini baadaye alianza kusisitiza jinsi uavyaji mimba ni afya ya uzazi... Mimi ni Mkatoliki. Mimi ni muungaji mkono wa maisha.

Tatizo ambalo nilikumbana nalo ni kwamba sijui jinsi Mkatoliki yeyote anavyoweza kumpigia kura mtu anayesema mambo kama vile tulivyoona [kutoka kwa Trump] huko Madison Square Garden hivi majuzi. Ninachukua suala la kumkaribisha mgeni na kumlisha nkumvisha kwa uzito sana.

Kwa hivyo chini ya hali hizo, sina mtu ninayeweza kumpigia kura.

Graphic with photo of Susana Rodriguez, 65, of Texas

Mkazi huyu mstaafu wa Texas alimpigia kura Biden katika uchaguzi uliopita wa urais na amepiga kura mapema kumuunga mkono Harris.

Napata hofu sana. Kwa kweli hatuwezi kurudi nyuma. Inanitisha sana. Nilikuwa na haki zaidi ya atakazokuwa nazo mjukuu wangu katika siku zake za usoni na hiyo si sawa.

Inasikitisha sana kwamba kuna ushindani mkali sana. [Trump] ni mhalifu aliye nje kwa dhamana. siwaelewi wanachama waRepublican. Walikuwa wakisimamia sheria na utaratibu [chama] na sasa hali ni hii.

Nafikiri [wanawake wengi] wanajitokeza na kusema, 'Kwa nini unatuambia nini cha kufanya na miili yetu?' Kutoa mimba ni jambo la kibinafsi na ni juu ya daktari na mwanamke. Si shughuli yangu'.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China