Mustakabali usiojulikana wa mgogoro wa Iran na Israeli

 

Mustakabali usiojulikana wa mgogoro wa Iran na Israeli

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Mgogoro kati ya Iran na Israel haujawahi kutokea katika historia ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na umesababisha eneo la Mashariki ya Kati kukabiliwa na hofu ya vita vya maangamizi.

Lakini wakati huo huo, maelezo ya kile kilichotokea yanaonyesha jinsi ushindi wa mwisho wa kijeshi usivyoweza kupatikana katika mapambano haya.

Iran haina uwezo wa kuishambulia Israel na kuiangamiza serikali ya nchi hiyo, wala Israel haiwezi kuiteka Tehran.

Kila moja ya nchi hizi ina sababu tofauti za kutenda kwa umakini. Hata hivyo, nchi zote mbili zinaogopa kupoteza sifa zao, na kwasababu hii, haziwezi kukaa muda bila kufanya shambulio lolote dhidi ya upande mwingine, na mvutano huu unaendelea.

Kutokana na hilo nchi hizo mbili zinatumia makombora ya masafa marefu na ndege za kivita za F-35, na zana nyingine za kivita.

Vita vya historia

Kama migogoro yote ya kimataifa, pande hizo mbili zina hadithi tofauti kabisa kuhusu mvutano huu wa kijeshi na wanajaribu kwa nguvu zao zote kuanzisha hadithi yao wanayoitaka wao kuielezea kama "ukweli" wa hadithi, sawa na watu wawili ambao hawakubaliani juu ya kitu na kusisitiza mahakamani kwamba upande mwingine ni waongo.

Israel inasema kuwa ilikabiliwa na shambulio kutoka kwa serikali ya Kiislamu isiyo ya kidemokrasia na kuanzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi katika kujilinda. Katika hadithi ambayo Israeli na wawakilishi wake wanaendeleza katika vyombo vya habari vya kimataifa na mitandao ya kijami- ni kwamba nchi hii ndio nchi ya "demokrasia pekee" katika Mashariki ya Kati ambayo inapambana dhidi ya serikali zisizo za kidemokrasia na za utawala wa kiimla za kanda.

Kwa simulizi ya Iran, Israel ni nchi inayovamia nchi nyingine inayokiuka sheria za kimataifa, ilishambulia ubalozi wa Iran nchini Syria, na kumuua Ismail Haniyeh, mgeni rasmi wa serikali, ndani ya nchi. Iran inasema kuwa ilirusha kombora kujibu hatua za Israel.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Picha ya Hassan Nasrallah karibu na Qassem Soleimani, Abu Mehdi Al-Muhandis na Ahmed Yassin katika moja ya mitaa ya Sana'a, mji mkuu wa Yemen

Kati ya nchi hizi mbili, Israel haikabiliwi na tatizo kubwa la kukuza hadithi yake inayotaka raia wake waiamini huku Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo iko katika mgogoro wa muda mrefu, wa vurugu na wa kiimla na kundi la raia wake, ikipata uungaji mkono wa maoni ya umma hauji bila changamoto.

Katika ngazi ya kimataifa, ushindani wa matangazo wa kujinadi kama wenye sababu bora za mapigano unaendelea kwa kiwango kikubwa kati ya Iran na Israeli.

Vita vya uchumi

Vita vinahitaji fedha. Na kwa pande zote mbili, gharama za kiuchumi za mgogoro huu na usimamizi wa rasilimali za nchi hizi mbili zinaweza kuwa na jukumu muhimu katika kuendeleza mvutano huu.

Kwa Iran, ambayo inakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi kutokana na vikwazo vya Marekani, mgogoro huu utakuwa ghali sana. Mbali na gharama za utengenezaji wa makombora na ndege zisizo na rubani, makundi ya wakala - hususan Hezbollah ya Lebanon, ambalo pia ilmepata pigo kubwa na lina mahitaji mengi - yana gharama.

Mbali na vitisho vya nje, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia inakabiliwa na upinzani mkubwa miongoni mwa raia.

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Viwango vya ubora wa maisha ya raia wa Israeli ni sawa na nchi tajiri za Ulaya kuliko nchi ya Mashariki ya Kati miongoni mwa majirani kama Misri, Jordan na Syria.

Lakini wakati huo huo, uchumi wa vita kwa Israeli ni karibu siri na kubwa. Ingawa uchumi wa Israel ni wa juu zaidi kuliko wa Iran, gharama za kijeshi za nchi hiyo pia ni kubwa sana.

Benjamin Netanyahu anasisitiza kuwa nchi hii inaweza kuwashinda maadui zake wote peke yake, lakini ukweli ni kwamba kama isingekuwa msaada wa kifedha na silaha kwa nchi za Magharibi, hasa Marekani, Israel ingekabiliwa na vikwazo vikali mwaka huu.

Kulingana na makadirio ya Wizara ya Fedha ya Israeli, vita huko Gaza viligharimu nchi hiyo dola bilioni 26.5 hadi mwisho wa Agosti (wiki ya pili ya Septemba).

Benki Kuu ya Israeli imetabiri kuwa gharama hizi zinaweza kufikia dola bilioni 70 ifikapo mwishoni mwa 2025.

Wakati huo huo, madeni ya kigeni ya Israeli yanaongezeka na kiwango cha mikopo ya nchi kimepungua katika masoko ya dunia.

Moja ya sababu za kuongezeka kwa gharama za vita kwa Israeli ni ngao ya ulinzi wa makombora ya Iron Dome na teknolojia nyingine za ulinzi wa makombora, ambazo ni ghali sana na zimetumiwa na Israeli wakati huu wote.

Vita vya mtandaoni na vita vya kiteknolojia

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel, tangu shambulio la Oktoba 7, mashambulizi ya kimtandao ya Iran dhidi ya Israel yameongezeka mara tatu. Mara kwa mara, kumekuwa na ripoti za vitendo vya makundi kama vile "CyberAveng3rs", ambayo Marekani inasema ina uhusiano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na hapo awali ilihusika katika mashambulizi ya kimtandao dhidi ya nchi hiyo.

Zaidi ya hayo teknolojia nyingine za hali ya juu zilizotengenezwa na IRGC kwa vita vya kiteknolojia zimeonyesha uwezo wao katika migogoro ya hivi karibuni. Mfano muhimu wa sekta hii ni ndege zisizo na rubani za kujitoa mhanga, ambazo, kwa mujibu wa vyanzo vya Marekani, zilitumika kwa kiasi kikubwa katika mashambulizi dhidi ya Israeli na kusababisha changamoto kubwa ya usalama kwa nchi hii.

Kwa upande mwingine, Israeli imechukua hatua kama hizo na imetumia teknolojia za kisasa katika vita na vikundi vya wakala na hata katika mapambano ya moja kwa moja.

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hamas, moja ya makundi yanayoungwa mkono na Iran, iliwateka nyara Waisraeli 251 na wageni katika shambulio la Oktoba 7

Vita vya wakala

Kipengele kingine muhimu sana cha mgogoro wa hivi karibuni kati ya Iran na Israeli ni vita vya wakala; ambapo vikundi vinavyoungwa mkono na upande mmoja vinasababisha shida kubwa ya usalama kwa upande mwingine. Kwa sababu hii, kinachoweza kuathiri matokeo ya mwisho ya mvutano huu zaidi ya mashambulizi ya moja kwa moja ya Iran na Israeli kwa kila mmoja ni hadhi ya vikundi vya wakala, mkakati wa Iran katika kusimamia vikundi hivi, na sera ya Israeli katika kushughulika nao.

Kwa sasa, pamoja na kundi la Hamas, ambalo linaungwa mkono kikamilifu na Iran, kundi la Islamic Jihad pia linafanya kazi Gaza kama kundi jingine la Kiislamu ambalo viongozi wake wana uhusiano wa karibu na mamlaka ya Iran ikilinganishwa na Hamas. Kundi la Hezbollah nchini Lebanon, ambalo lilianzishwa kwa msaada wa Iran, pia liko vitani na Israel.

Mbali na makundi hayo, Iran pia inayahesabu makundi kadhaa ya wanamgambo wa Kishia nchini Iraq. Makundi haya kwa ujumla hutumiwa kushambulia maeneo ya Marekani. Kundi la Wahouthi la Yemen pia linajulikana kama mshirika mwingine wa Tehran, ambalo lilionyesha wakati wa vita vya Gaza ni kiasi gani linaweza kuathiri usalama wa Bahari ya Shamu na Bab al-Mandab.

Lakini kwa upande mwingine, nguvu ya Iran katika eneo hilo imeongezeka kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande mwingine, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaonekana kuwa mhusika pekee katika eneo hilo ambaye hayuko tayari kushindwa na Israeli.

Ingawa imani hii si sahihi, imeleta mambo muhimu kwa Tehran na wanadiplomasia wa Tehran wanafahamu kikamilifu mambo haya.

Vita visivyoonekana na mustakabali usio na uhakika

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Propaganda za chuki dhidi ya Israel zimefikia kilele kisicho cha kawaida nchini Iran mwaka jana

Katika hotuba za viongozi wa Iran na Israeli, kuna mazungumzo ya mara kwa mara ya "ushindi wa mwisho" na "kumshinda adui"; Maelezo ambayo yanaonekana kuwa na maana wazi kwa wasemaji, lakini kwa kweli ni ahadi za kisiasa ambazo hazitarajiwi kusababisha vita kamili.

Hata hivyo, moja ya malengo muhimu ya hatua za kijeshi za Iran na Israel dhidi ya kila mmoja ni kujenga kizuizi na kuongeza usalama, na hakuna nchi yoyote kati ya hizo mbili iliyofanikiwa kufikia lengo hili.

Kushinda vita hii ya propaganda ni muhimu tu, ingawa sio muhimu sana, kuliko vita vya kijeshi.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China