Naim Qassim: Mfahamu kiongozi mpya wa Hezbollah
Naim Qassim: Mfahamu kiongozi mpya wa Hezbollah

Chanzo cha picha, Getty Images
Hezbollah imetangaza uteuzi wa Amin Qassem kama katibu mkuu wa chama, kumrithi Hassan Nasrallah, mwezi mmoja baada ya mauaji yake katika uvamizi wa Israel ambao ulilenga makao makuu ya uongozi wa kundi hilo kusini mwa mji mkuu wa Lebnon, Beirut mwishoni mwa Septemba.
Naim Qasim ni nani?
Kwa mujibu wa kanuni za ndani za Hezbollah, naibu katibu mkuu wa chama humwakilisha katibu mkuu iwapo kutatokea dharura yoyote ya kisiasa au kiusalama. Ikitokea kifo cha katibu mkuu, naibu wake ameidhinishwa kutekeleza majukumu yake hadi mkutano wa dharura wa Shura utakapofanyika ambapo kiongozi mpya atachaguliwa kushika nafasi ya katibu mkuu wa chama.
Kwa sasa Qassem anashikilia wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu wa Hezbollah, chama cha kisiasa, kijeshi na kijamii ambacho kina msingi maarufu na ushawishi mkubwa miongoni mwa jamii ya Washia nchini Lebanon.
''Mwana wa Kafr Fila''

Chanzo cha picha, Reuters
Naim bin Muhammad Naim Qasim, alizaliwa Februari 1953 katika eneo la Basta al-Tahta mjini Beirut. Ameoa na ana watoto sita, wavulana wanne na wasichana wawili. Baba yake Muhammad alizaliwa katika mji wa Kfar Fila katika eneo la Iqlim al-Tuffah kusini mwa Lebanon.
Alisoma hadi ngazi ya juu ya masomo ya kidini, chini ya wanazuoni mashuhuri wa Kishia huko Lebanon. Kando na elimu ya kidini Naim pia alisomea shahada ya Kemia katika Chuo Kikuu cha Lebanon mwaka 1971.
Qassem pia alisomea shahada ya uzamili ya kemia katika Chuo Kikuu cha Lebanon mwaka wa 1977. Alifanya kazi kama mwalimu kwa madarasa ya sekondari ya umma kwa miaka sita, kwa kuwa ni mhitimu wa Chuo cha Ualimu kilichohusishwa na Wizara ya Elimu.
Alisoma vitabu vingi vya Kiislamu, ambavyo vilimpatia uzoefu wa kuzungumza hadharani na kuandaa masomo ya kidini katika umri mdogo. Baada ya hapo aliazna kuwafunza watoto kwa vipindi vya kadhaa kila wiki akiwa na umri wa chini ya miaka 18 wakati huo.
Alichangia kuanzishwa kwa "Muungano wa Wanafunzi wa Kiislamu wa Lebanon" na kikundi cha vijana wakati alipokuwa katika madarasa ya chuo kikuu, kwa lengo la kazi ya wanafunzi na kuwasilisha mawazo ya Kiislamu ndani ya vyuo vikuu na shule, mwanzoni mwa miaka ya sabini.
Mmoja wa waanzilishi wa vuguvugu la Amal
Alijiunga na Harakati za Brigedi za Upinzani wa Lebanon (Amal) ilipoanzishwa na Imam Musa al-Sadr mnamo 1974, na alihudhuria mikutano ya kwanza ya kuzindua vuguvugu hilo katika mikoa tofauti ya Lebanon, na kushikilia wadhifa wa Naibu Afisa wa Utamaduni katika Harakati ya Amal.
Alipanda ngazi ya arakati hizo akisimamia mafundisho na utamaduni, kwa sababu alikuwa mmoja wa makatibu wa baraza la uongozi wa Amal baada ya Imam al-Sadr kutoweka nchini Libya, na Bwana Hussein al-Husseini kuteuliwa katika uongozi wa Jumuiya ya Madola mnamo 1978.
Alijiondoa katika harakati hiyo kufuatia Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyofanywa na Khomeini Februari 11, 1979 ili kuendelea na masomo yake ya kidini na shughuli zake za kuendesha mihadhara katika misikiti kadhaa na Husseiniya huko Beirut na vitongoji vya kusini.
Kwa zaidi ya miaka 20, Naim Qassem amekuwa akifanya "mihadhara" kote Lebanon, akizingatia masomo ya kila wiki na mwongozo katika maeneo tofauti ya Beirut.
Alichangia kuanzishwa kwa Jumuiya ya Elimu ya Dini ya Kiislam ya “Shiite” mwaka 1977 inayojishughulisha na ufundishaji wa masuala ya Dini ya Kiislamu katika shule za serikali na za binafsi, kwa kupeleka walimu wa kike na kiume katika kila shule kutoa masomo ya dini katika ngazi zote.
Pia alishikilia wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa shule sita za Al-Mustafa katika vitongoji vya kusini vya Beirut, Tyre, Nabatieh na Qasr Nabaa, zinazofundisha mtaala rasmi wa Lebanon hadi 1990, huku akiendelea kufanya kazi katika chama.
Qassim alishiriki katika kamati za Kiislamu zinazounga mkono Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, ambazo zilijumuisha vikundi vyote vya Kiislamu vilivyokuwa vinafanya kazi katika eneo la tukio wakati huo, na ambazo ziliendesha shughuli za vyombo vya habari, maandamano na mihadhara kuhusu mapinduzi hayo.
Kuanzishwa kwa Hezbollah
Baada ya mikutano kati ya kamati za Kiislamu na Chama cha Islamic Dawa, tawi la Lebanon, na wanazuoni wa Bekaa na Harakati ya Kiislamu ya Amal mnamo 1982, Hezbollah ilianzishwa, na Naim Qassem alikuwa mmoja wa washiriki waanzilishi katika mikutano hii iliyochangia kuanzishwa kwa Hezbollah.
Alikuwa mjumbe wa Baraza la Shura la chama kwa mihula mitatu, mwanzoni akichukua jukumu la shughuli za elimu na skauti huko Beirut, kisha kama Naibu Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu, na hatimaye kama Mwenyekiti wake.
Alishika wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu wa Hezbollah tangu Abbas al-Moussawi alipokuwa Katibu Mkuu wa chama mwaka 1991, na kuhudumu katika wadhifa huo baada ya mauaji ya al-Moussawi, ambaye alirithiwa na Katibu Mkuu aliyeuawa, Jenerali Sayyed Hassan Nasrallah, mwaka 1992.
Qassem pia anaongoza Baraza la Utekelezaji la Bunge la Hezbollah, ambalo linafuatilia Uaminifu kwa Kambi ya Upinzani, kazi ya kutunga sheria ya manaibu, na harakati zao za kisiasa.
Kutokana na nafasi yake katika uongozi wa Hezbollah, Naim Qassem anaongoza kazi ya kisiasa, na anazungumza sana na vyombo vya habari na kushiriki mahojiano na mihadhara.
Amekuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Katibu Mkuu wa Hezbollah Hassan Nasrallah, kwa zaidi ya miaka 35 kupitia nafasi ya pamoja ya kiutendaji katika Baraza la Shura la chama, mikutano ya kudumu na mashauriano.