Sean 'Diddy' Combs akabiliwa na kesi mpya za kuwanyanyasa wavulana kingono

 

Sean 'Diddy' Combs akabiliwa na kesi mpya za kuwanyanyasa wavulana kingono

Diddy

Chanzo cha picha, Reuters

Sean 'Diddy', Rapa mwenye umri wa miaka 54 anadaiwa kumpiga mvulana mmoja ambaye alisafiri na familia yake kwa ajili ya mikutano na wakuu wa tasnia ya muziki, katika chumba cha hoteli mjini New York mwaka 2005.

Sean "Diddy" Combs ameshtakiwa kwa kumpa dawa za kulevya na kumdhalilisha kingono mvulana wa miaka 10 katika kesi mpya.

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 54, anadaiwa kumvamia mvulana huyo katika chumba cha hoteli mjini New York mwaka wa 2005.

Kesi ya pili mpya inamtuhumu gwiji huyo wa muziki wa hip-hop anayeshikiliwa jela kwa kumshambulia kijana mwenye umri wa miaka 17 ambaye alishiriki katika kipindi cha televisheni cha Making the Band mwaka wa 2008.

Ni shutuma za hivi karibuni katika wimbi la kesi ambapo washtaki wanadai walinyanyaswa kingono na Combs kwenye karamu na mikutano katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Wanasheria wa Combs walikanusha madai hayo mawili mapya na kumshutumu wakili wa walalamikaji, Anthony Buzbee, kwa kutaka.

Bw Buzbee anasema anawakilisha zaidi ya waathiriwa 150 wa rapa huyo, na amewasilisha takribani kesi 17.