Shughuli za uokoaji zinaendelea huku Uhispania ikiomboleza vifo vya takriban watu 100

 

Shughuli za uokoaji zinaendelea huku Uhispania ikiomboleza vifo vya takriban watu 100

.

Chanzo cha picha, EPA

Uhispania inakabiliana na athari mbaya ya mafuriko ambayo yaliathiri jamii za kusini katika saa 24 zilizopita.

Taarifa ya mwisho kutoka kwa mamlaka ya Valencia saa 19:30 CET (18:30 GMT) ilisema idadi ya waliofariki katika eneo hilo ni 92, na watu wengine wawili waliuawa katika eneo jirani la Castilla-La Mancha.

Muingereza mwenye umri wa miaka 71 pia alifariki saa chache baada ya kuokolewa kutoka nyumbani kwake Alhaurin de la Torre, huko Malaga, kulingana na kiongozi wa eneo la Andalusia.

Mwanahabari wetu Nicky Schiller ametua tu Valencia na anasema mvua imepungua, lakini hapo awali, Waziri Mkuu Pedro Sanchez aliwataka wakaazi katika eneo hilo, na pia wa Andalusia na Catalonia, kuwa waangalifu kwani maonyo ya hali ya hewa bado yanaendelea katika maeneo mengi.

Waziri wa sera za eneo Ángel Víctor Torres alisema bado haijulikani ni watu wangapi walipoteza maisha baada ya mvua kubwa mno kunyesha kusini mwa Uhispania katika muda wa saa nane siku ya Jumanne.

Na kama Mfalme Felipe wa Sita alivyozungumzia "uharibifu mkubwa" uliosababishwa na mafuriko, Torres alitangaza Uhispania itaadhimisha siku tatu za maombolezo kuanzia kesho hadi Jumapili. Wakati huo huo, shughuli za utafutaji na uokoaji zitaendelea.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China