'Sote tunajua mtu ambaye amefariki dunia – hili ni jinamizi'
'Sote tunajua mtu ambaye amefariki dunia – hili ni jinamizi'
Hapa Paiporta, Valencia, ambapo makumi ya watu waliuawa katika mafuriko ya ghafla, maduka, nyumba na biashara zimeharibiwa.
Katika mtaa mmoja naona watu wakiopoa maiti.
Akiwa amesimama nje ya mabaki ya duka lake la dawa, mfamasia Miguel Guerrilla ananiambia: "Sote tunamfahamu mtu ambaye amefariki dunia."
"Hili ni jinamizi," anasema.
Watu waliojitolea wamefika kusaidia kusafisha lakini ni kazi ya kutisha. Ninapotembea kijijini, nimeona gari la huduma ya mazishi limefika kuchukua mwili mwingine.