Takriban watu 93 wameuawa katika shambulizi la Israel huko Gaza - Hamas

 

Takriban watu 93 wameuawa katika shambulizi la Israel huko Gaza - Hamas

.

Chanzo cha picha, Reuters

Takriban watu 93 wamefariki au hawajulikani walipo baada ya kutokea kwa mashambulizi ya anga ya Israel katika mji wa Beit Lahia kaskazini mwa Gaza, wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas imesema.

Waokoaji walisema jengo la makazi la ghorofa tano lilishambuliwa, na video kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha miili iliyofunikwa kwa blanketi sakafuni.

Hakujakuwa na maoni ya mara moja kuhusu shambulizi hilo kutoka kwa jeshi la Israel, ambalo lilianza mashambulizi mapya katika eneo hilo mapema mwezi huu baada ya kusema Hamas inajipanga upya huko.

Vikosi vya Ulinzi vya Israel vimekuwa vikiendesha shughuli zake kaskazini mwa Gaza katika muda wa wiki mbili zilizopita, hasa katika maeneo ya Jabalia, Beit Lahia na Beit Hanoun.