Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 31.10.2024
Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 31.10.2024
Ruben Amorim tayari amezungumzia mipango yake ya uhamisho na uongozi wa Manchester United na haoni winga Antony, viungo Casemiro na Christian Eriksen au beki Victor Lindelof kama sehemu ya mipango yake. (TeamTalks)
Jitihada za United kupata huduma ya Amorim zimegonga mwamba baada ya Sporting kudai pauni milioni 4 kwa wafanyikazi wake pamoja na ada ya kuachiliwa kwa meneja huyo ya pauni milioni 8.3. (Times – Subscription Required)
Amorim anakubali huenda akalazimika kusubiri hadi mapumziko ya kimataifa mwezi ujao ili kujiunga na United. (Telegraph – Subscription Required)
Uamuzi wa West Ham kutomteua Amorim msimu uliopita ulitokana na kutokuwa na uzoefu wa kusimamia klabu kubwa, badala ya kifedha. (Daily Mail), nje
Barcelona wanavutiwa na winga wa AC Milan Rafael Leao, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 25 kwa sasa akiwa hapendezwi na San Siro. (Sport – Via Spanish)
Manchester City imekataa mipango ya klabu kadhaa kumchukua kiungo mshambuliaji Claudio Echeverri, 18, kwa mkopo huku Muargentina huyo akitarajiwa kuungana na kikosi cha Pep Guardiola kutoka River Plate mwanzoni mwa 2025. (Fabrizio Romano),
Roma wameanza kutafuta meneja mbadala iwapo kocha wa sasa Ivan Juric atashindwa kushinda mechi yao ijayo dhidi ya Torino. (Corriere dello Sport – In Italyo)
Erik ten Hag alifikiria kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Danny Welbeck, ambaye sasa ana umri wa miaka 33, kutoka Brighton wakati wa uongozi wake kama meneja wa Mashetani Wekundu. (The Athletic – Subscription Required).
West Ham watakuwa na shida kuendeleza nia yao ya kumnunua fowadi wa Atalanta Ademola Lookman, 27, huku Paris St-Germain wakipewa nafasi kubwa ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria iwapo atapatikana. (Football Insider)
Real Madrid watafikiria kumnunua beki wa pembeni wa Tottenham na Uhispania Pedro Porro, 25, ikiwa hawataweza kukamilisha uhamisho wa mlinzi wa Uingereza na Liverpool Trent Alexander-Arnold. (AS – In Spanish)
Klabu za Saudi Pro League zinasalia kuwa na hamu ya kumsajili fowadi wa Brazil Vinicius Junior, 24, kutoka Real Madrid, wakitumai mchezaji huyo atakuwa amechoshwa na soka la Ulaya baada ya kunyimwa tuzo ya Ballon d'Or. (Sport – In Spanish)
Mshambuliaji wa Ujerumani Thomas Muller, 35, ana nia ya kutaka kuhamia Ligi Kuu ya Soka atakapoondoka Bayern Munich. (Bild – In Deutch)
Napoli wanaendelea na mazungumzo na fowadi wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 23, kuhusu kandarasi mpya, ambayo itajumuisha kifungu cha kununua cha £84m (euro milioni 100). (Sky Sports Italia – in Italia)