‘Tunaomba Malkia wa urembo Muheto afungwe mwaka mmoja’ - Mwendesha Mashtaka

 

‘Tunaomba Malkia wa urembo Muheto afungwe mwaka mmoja’ - Mwendesha Mashtaka

.

Chanzo cha picha, Miss Rwanda

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka nchini Rwanda amemuombea Malkia wa urembo wa Rwanda Divine Muheto kifungo cha mwaka mmoja na miezi minane kwa makosa ya kuendesha gari akiwa amekunywa pombe kupita kiasi, na kugonga miundombinu kisha kutoroka eneo la tukio.

Bi Muheto, 21, alifikishwa mahakamani mapema Alhamisi asubuhi, saa chache kabla ya kesi kuanza kusikilizwa.

Chumba kidogo cha Mahakama ya mtaa ya Kicukiro kilijaa wanahabari wengi na watu walioonekana kuwa marafiki na wanafamilia wake.

Baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili, Divine Muheto ambaye alikuwa akiwakilishwa na mawakili watatu, alisema anakiri kosa la kuendesha gari akiwa mlevi na kugonga na kukimbia.

Kwa sauti ndogo, akionekana kuwa mwenye hofu, alisema: “Lakini siamini kwamba nilitoroka kwasababu gari nililiacha hapo. Niliogopa kwa sababu watu wengi walikusanyika na kuhofia kwamba wangeniumiza. Polisi walipofika nilirudi peke yangu.”

Upande wa mashtaka ulisema kuwa makosa yanastahili adhabu wanayomuombea. Pia ilisema kuwa Muheto alikuwa na kiwango kilevi hadi point 4 huku kiwango cha pombe cha kinachokubaliwa kikiwa ni kipimo cha point ni 0.8.

Ilitangazwa mahakamani kuwa Muheto alikamatwa Jumapili, Oktoba 20, lakini ni Jumanne, Oktoba 29 ndipo polisi walipotangaza kwamba alikamatwa.

.

Chanzo cha picha, Divine Muheto akishuka kwenye gari la mahabusu wakati alipofikishwa katika mahakama ya Kicukiro mjini Kigali.

Mawakili wake walisema hawaoni ni kwanini mteja wao amekuwa mahabusu muda wote huo na kufikishwa mahakamani, kwamba wanaona ni tofauti na watu wengine wanaofanya uhalifu unaofanana na huo na kupigwa faini na kufungwa kwa siku tano, kisha kuachiwa.

Mawakili wake waliomba Muheto aachiliwe na kutozwa faini huku akiomba msamaha na kukiri baadhi ya mashtaka.

Muheto pia alisema: "Nimefungiwa kwa siku 11 na kulia, sitarudia uhalifu huo."

Hakimu huyo alisema baada ya kusikiliza pande zote mbili tarehe 6 Novemba, mahakama itasoma uamuzi.

Muheto bado anashikiliwa na polisi.

Muheto alipata umaarufu mwaka 2022 aliposhinda Malkia wa Urembo wa Rwanda.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China