Uingereza na nchi nyingine nane 'zasikitishwa' na visa vya utekaji nyara nchini Kenya

 

Uingereza na nchi nyingine nane 'zasikitishwa' na visa vya utekaji nyara nchini Kenya

Mabalozi tisa na makamishna wakuu wa balozi za kigeni nchini Kenya wameelezea wasiwasi wao kutokana na visa vya hivi majuzi vya utekaji nyara kote nchini.

Denmark, Finland, Ujerumani, Ireland, Uholanzi, Norway, Uswidi, Uswizi na Uingereza katika taarifa ya pamoja siku ya Alhamisi zilisema kila Mkenya ana haki na uhuru wa kimsingi zilizolindwa katika katiba.

"Kulinda haki za binadamu kunaleta utulivu na ustawi. Kwa hivyo, tuna wasiwasi juu ya ripoti zinazoendelea za kukamatwa kwa watu kiholela na kutoweka licha ya maamuzi ya Mahakama Kuu,"

"Ni muhimu kuhakikisha utawala wa sheria unatawala na maamuzi ya mahakama yanafuatwa."

Mabalozi na makamishna wakuu walirejelea ahadi ya mara kwa mara ya Rais William Ruto tangu ashike wadhifa wake mwaka wa 2022 kwamba visa vya watu kutoweka havitafanyika chini ya uangalizi wake.

Huku wakipongeza Kenya kwa kuchaguliwa kwake katika Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, wajumbe hao wametaka uchunguzi ufanyike kuhusu utekaji nyara huo.

"Uchunguzi wa haraka na wa wazi utaiwezesha Kenya kuonyesha kwa Ulimwengu kujitolea kwake kudumisha haki inapochukua nafasi yake katika Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa," walisema.

Katika wiki za hivi majuzi, waomba hifadhi saba kutoka Uturuki walitekwa kikatili na maafisa wa usalama jijini Nairobi, na hivyo kuzua shutuma kutoka kwa makundi ya kutetea haki za binadamu.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China