Urusi yatoza Google faini ya thamani ya pesa isiyoweza kuhesabika
Urusi yatoza Google faini ya thamani ya pesa isiyoweza kuhesabika
Mahakama ya Urusi imeitoza Google faini ya thamani isiyoweza kuhesabika - mbili zikifuatwa na sufuri 36 - kwa kuzuia vituo vya habari vya serikali ya Urusi kwenye YouTube.
Kwa dola hiyo inamaanisha kuwa kampuni hiyo kubwa ya kiteknolojia ameambiwa alipe $20,000,000,000,000,000,000,000,000,000,000,000.
Licha ya kuwa moja ya kampuni tajiri zaidi duniani, hiyo ni zaidi ya dola trilioni 2 za thamani ya Google.
Kwa hakika, ni kiasi kikubwa zaidi kuliko jumla ya Pato la Taifa la dunia, ambalo linakadiriwa na Shirika la Fedha la Kimataifa kuwa $110 trilioni.
Faini hiyo imefikia kiwango cha juu sana kwa sababu - shirika la habari la serikali Tass linasema - inaongezeka maradufu kila siku ambayo haijalipwa.
Kulingana na Tass, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alikiri "hawezi hata kutamka nambari hii" lakini akahimiza "wasimamizi wa Google kuzingatia."
Kampuni hiyo haijatoa maoni hadharani au kujibu ombi la BBC la taarifa.