Waziri wa Israel asema uteuzi wa kiongozi mpya wa Hezbollah ni 'wa muda'

 

Waziri wa Israel asema uteuzi wa kiongozi mpya wa Hezbollah ni 'wa muda'

.

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock

Kwingineko, Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant, ameweka ujumbe kwenye mtandao wa X kuhusu kiongozi mpya wa Hezbollah Sheikh Naim Qassem, na kusema: "Uteuzi huo ni wa muda. Sio wa kudumu."

Kauli ya Gallant inawadia baada ya wanajeshi wa Israel kuua idadi kubwa ya viongozi wa Hezbollah katika wiki chache zilizopita, akiwemo kiongozi wa muda mrefu Hassan Nasrallah, ambaye aliuawa katika shambulio kubwa la anga la Israel huko Beirut mwezi Septemba.

Hezbollah ilitangaza uteuzi wa Qassem mapema leo, ikimtaja kama "aliyebeba bendera iliyobarikiwa katika maandamano haya".