Waziri wa Ulinzi wa Marekani asema wanajeshi wa Korea Kaskazini wamevalia sare za kijeshi za Urusi

 

Waziri wa Ulinzi wa Marekani asema wanajeshi wa Korea Kaskazini wamevalia sare za kijeshi za Urusi

..

Chanzo cha picha, KCNA/Uriminzokkiri

Maelezo ya picha, .

Mawaziri wa ulinzi wa Marekani na Korea Kusini, Lloyd Austin na Kim Yong Hyun, walifanya mkutano na waandishi wa habari mjini Washington.

Wakizungumza juu ya Korea Kaskazini, haswa utumaji wake wa wanajeshi kwenda Urusi ambapo Moscow na Pyongyang hawakatai hatua hiyo, ingawa hawakubali moja kwa moja.

Austin alisema wanajeshi wa Korea Kaskazini waliotumwa Urusi wamebadilika na kuanza kuvaa sare za kijeshi za Urusi, taarifa iliyotolewa mapema Jumatano kwenye kikao na Baraza la Usalama la Kitaifa la Korea Kusini.

Austin pia alisema hata kwa msaada wa Korea Kaskazini, Urusi haitaishinda Ukraine.

Marekani na washirika wake wataihamasisha Pyongyang kutotumia wanajeshi hao katika shughuli za kijeshi, lakini aliweka bayana kuwa hii inaweza kutokea hata hivyo.

Kim Yong Hyun alitoa wito kwa Korea Kaskazini "kuondoa mara moja" wanajeshi wake wote kutoka Urusi.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China