Mashirika ya ndege ya India yamekumbwa na vitisho 1,000 vya uongo vya mabomu
Mashirika ya ndege ya India yamekumbwa na vitisho 1,000 vya uongo vya mabomu

Chanzo cha picha, Getty Images
Mashirika ya ndege na viwanja vya ndege vya India vilipokea vitisho 999 vya uongo mashambulio ya mabomu mwaka huu kufikia tarehe 14 Novemba, naibu waziri wa usafiri wa anga wa nchi hiyo aliliambia bunge lake.
Hii ilikuwa karibu mara 10 zaidi ya vitisho vilivyopokelewa mnamo 2023, Bw Murlidhar Mohol alisema.
Zaidi ya vitisho 500 vya mwaka huu vilipokelewa katika wiki mbili zilizopita za mwezi Oktoba.
Ongezeko kubwa la vitisho vya uongo lilikuwa limesababisha uharibifu kwenye ratiba za ndege, na kusababisha usumbufu mkubwa katika mpango wa utoaji huduma.
Vitisho vya hivi majuzi vyote ni uwongo, Bw Mohol alisema, na "hakuna tishio halisi lililogunduliwa katika viwanja vya ndege nchini India".
Polisi wamepokea malalamiko 256 na watu 12 wamekamatwa kuhusiana na vitisho hivi, waziri alisema.
Lakini visa hivyo vinaashiria ongezeko ambalo halijawahi kushuhudiwa vya matukio kama hayao.
Kati ya 2014 na 2017, viongozi walikuwa wamerekodi arifa 120 za uongo za mabomu kwenye viwanja vya ndege, na karibu nusu zilielekezwa Delhi na Mumbai, viwanja vya ndege vikubwa zaidi nchini.