Mwanamuziki wa Mali azuiliwa nchini Ubelgiji kutokana na mzozo wa malezi ya mtoto

 

Mwanamuziki wa Mali azuiliwa nchini Ubelgiji kutokana na mzozo wa malezi ya mtoto

h

Chanzo cha picha, Reuters

Mmoja wa wanamuziki mashuhuri barani Afrika wa Mali Rokia Traoré ameripotiwa kufungwa nchini Ubelgiji kama sehemu ya mzozo unaoendelea wa malezi ya mtoto.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 50 amezuiliwa baada ya kurejeshwa kutoka Italia, kwa ajili ya kifungo cha miaka miwili jela, kulingana na shirika la habari la AFP.

Sakata hiyo ya muda mrefu ilianza 2020 wakati Traoré aliwekwa kizuizini nchini Ufaransa kutokana na hati ya kukamatwa ya Ubelgiji baada ya kushindwa kutii amri ya mahakama ya kumkabidhi binti yake kwa baba wa msichana huyo kutoka Ubelgiji.

Miezi kadhaa baada ya kuachiliwa kwa masharti , Traoré alisafiri hadi Mali kwa ndege ya kibinafsi, akikaidi marufuku ya kuondoka Ufaransa hadi aliporejeshwa Ubelgiji.

Oktoba mwaka jana, Traoré alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela bila kuwepo mahakamani na mahakama nchini Ubelgiji kwa tuhuma za utekaji nyara wa mzizi kwa "kukosa kumkabidhi mtoto kwa mtu anayestahili kumlea"

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China