'Nilimuuzia nyumba mtu aliyekuwa akisakwa na FBI'
'Nilimuuzia nyumba mtu aliyekuwa akisakwa na FBI'

Chanzo cha picha, Aled Evans
Mwanamume mmoja ambaye alimuuzia nyumba yake mtu ambaye alibainika kuwa kwenye orodha ya watu wanaotafutwa sana na FBI amesema kuwa hilo lilikuwa eneo linalofaa "ikiwa ungetaka kujificha.
Daniel Andreas San Diego alilipa pauni 425,000 kwa ajili ya nyumba hiyo karibu na Llanrwst kaskazini mwa Wales mnamo Agosti 2023 akitumia jina la Danny Webb.
Siku ya Jumatatu, Bw San Diego - ambaye kitita cha $250,000 (£199,000) kilitangazwa kwa atakayefanikisha kutoa taarifa zake,alikamatwa huko Maenan baada ya miaka 21 ya kukimbia kufuatia milipuko miwili huko San Francisco mnamo 2003 ambayo alishukiwa kuhusika.
"Alifurahi sana kwa sababu kulikuwa na msitu mkubwa nyuma ya nyumba, alikuwa akiendesha baiskeli yake na hiyo ndiyo iliyomuuzia," alisema Aled Evans.
"Ilionekana kama mahali pazuri alipopataka - lakini alitaka kwa sababu zake nyingine," aliiambia BBC Radio Wales
Daniel San Diego alipatikana wapi?
Maenan anakaa nje kidogo ya mtaa A470, mojawapo ya barabara kuu zinazopitia Wales kaskazini, kama maili 10 (16km) kutoka Conwy.
Ni jumuiya inayosambaa yenye mashamba na nyumba ndogo zilizotengwa, nyingi ambazo sasa ni nyumba zinazotumika nyakati za mapumziko ya likizo.
Hakuna duka au baa ya kijijini.
Makazi mengi utakayopishana nayo kwenye njia ya kwenda Llidiart y Coed yanaonekana kuwa nyumba zinazotumika nyakati za likizo.
Majirani Wawili kati ya wale ambao wanaishi karibu na makazi hayo waliripoti kumuona mara chache au kutoonana kabisa na mwanamume ambaye amekuwa akisakwa kwa miaka 20.
Mmoja alitambua gari jeusi la Seat Leon lililoegeshwa karibu kuwa mali ya San Diego.
Wala hakuonekana kuwa na mawasiliano yoyote ya moja kwa moja naye.

Nyumba inayozungumziwa ni nyeupe iliyo na kibaraza yenye mandhari ya kuvutia ya vilima na bustani iliyotunzwa vizuri.
Wakati BBC ilipotembelea, rundo la funguo lilikuwa likining'inia kwenye kufuli la mlango wa kioo kwa ndani, huku sufuria na vyombo vilikuwa vimetawanywa juu ya sinki la jikoni.
Unakaribishwa na ujumbe wa chaki kwenye ubao unapotembea kwenye njia ya bustani iliyoachwa kwa watu wa binmen zaidi ya mwaka mmoja uliopita na familia ya watu wanne ambao waliishi hapa awali.
Inaonekana kwamba Bw San Diego hakuwa na haraka ya kufanya mahali pale pawe pake.
Ndani tu ya mlango jozi ya visima vizito vilionekana vikiwa vimetelekezwa kati ya rundo ndogo la nguo, nguzo ambayo haijafunguliwa na zana za hali ya juu.
Dalili zote ni kwamba hii ilikuwa nyumba ambayo – kwa mujibu wa upelelezi –iliachwa kwa ghafla.
Bw Evans alisema nyumba hiyo ilikuwa kwenye "njia yenye shughuli nyingi".
Aliongeza kuwa Bw San Diego alitoa pauni 15,000 zaidi ya bei iliyotakiwa.
"Siku ya kukagua alitumia muda mwingi kwenye baraza akitazama mandhari na hivyo ndivyo nilivyomuuzia," Bw Evans alisema.
Aliiambia BBC kwamba "Danny" alifurahi kutumia pori lililo nyuma ya nyumba kwa kuendesha baiskeli mlimani, lakini alifikiri ni ajabu kwamba hakuonekana kuwa na wasiwasi kuhusu kazi ambayo haijakamilika ya ukarabati wa nyumba iliyoharibiwa na majira ya joto.
Bw Evans alimuelezea Bw San Diego kama mtu mwema, mtulivu ambaye alimwambia kuwa kazi yake ya IT imemleta Wales.
"Nilidhani yeye ni raia wa Canada na si Mmarekani," alisema, akimwelezea kuwa anazungumza kwa upole.
Aliiambia BBC Radio Cymru's Dros Frecwast kwamba alimwona Bw San Diego kwa takriban dakika 20 siku aliyohamia.
"Hakuwa na haraka na alikuwa mtulivu sana wakati wote," na kuongeza majirani "hawakuwahi kumwona".
Aligundua kuhusu kukamatwa kwa Bw San Diego baada ya jirani yake wa zamani kumpigia simu kumwambia taarifa hizo za kushtua.
"Haijazama bado. Lakini haijatuathiri, bila shaka. Hungeweza kuhimili.
Bado Lakini haijatuathiri, bila shaka. Isingewezekana.
"Palikuwa mahali pazuri pa kujificha na alivutiwa na muonekano wa nyumba hiyo. Muonekano wa siku zijazo hautakuwa mzuri hata kidogo’’

Mshirika wa Bw Evans, Suzanne Thomas alisema anakumbuka kufanya mazungumzo na Bw San Diego, akimtaja kama "mpenzi mzuri sana".
Aliongeza:"Ninajua kuwa makazi yake yalikuwa Mold wakati huo, nadhani ndivyo alivyosema.
"Ilikuwa kana kwamba amepata mahali pake, ukipenda. Nadhani alipapenda kweli."
Hata hivyo, alikiri kuwa na mashaka namna wakili wa Bw San Diego hakuulizia gharama au mahitaji mengine ya kawaida yaliyohusika katika ununuzi wa nyumba.
Bi Thomas alisema alikuwa amepata marafiki katika eneo hilo, ingawa, "Leo asubuhi nilizungumza na mwanamke mmoja, kwa bahati.
"Nilisema kilichotokea kwenye nyumba yetu na akasema 'ninamjua, Danny Webb'.
"Alisema aliwahi kuwa naye kwenye baa, mumewe alikuwa ameenda kupanda naye mlima. Walitumia muda mwingi pamoja katika miezi michache iliyopita.
"Ni wazi alikuwa akishirikiana na kufurahia mazingira."
FBI hatimaye ilimpata mtu huyo akiishi mwishoni mwa njia ndefu, nyembamba ambayo ilitumiwa na watembea kwa miguu kwenye mlima wenye misitu minene inayoelekea eneo maarufu kutazama la Cadair Ifan Goch na mwonekano mzuri unaopatikana kote Milima ya Carneddau ya Eryri.
Llidiart y Coed hunufaika kutokana na mandhari nzuri ya kuvutia.
Maeneo makubwa ya mto Conwy yanaonekana wazi chini, yakielekea baharini maili chache kuelekea kaskazini, huku taswira yenye barafu wy Carnedd Llewelyn ikionekana kumetameta kwa mbali.
Ni sauti ya magari inayosikika kwa mbali kutoka kwenye Barabara ya A470 hukukumbusha jinsi ulivyo karibu na maisha ya mjini.
Llidiart y Coed hapo zamani ilikuwa jumba la ghorofa mbili la Wales. Lakini upanuzi mkubwa wa paa la ghorofa moja, iliyozingirwa na baridi ya mwishoni mwa Novemba, sasa hutoa eneo kuu la kuishi.
Taarifa za namna mwanamume huyo anayejulikana mahali hapo kama Danny Webb alivyoishi katika makazi haya ya Wales, huenda zitaibuka katika siku zijazo.
Kuna maoni kwamba alikuwa mwendesha baiskeli mlimani na nguo aliyoning’iniza nyuma ya mlango ilionyesha mtu ambaye alifurahiya sana shughuli za nje.
Lakini baada ya miaka 20 ya kujificha, makazi yajayo ya Daniel Andreas San Diego, huenda yakawa gerezani, itakuwa tofauti sana.

Kwa nini FBI walimsaka Daniel San Diego?
FBI imemshutumu Bw San Diego kwa kuwa "mtu mwenye msimamo mkali kuhusu haki za wanyama" aliyehusika katika mfululizo wa shambulio la mabomu huko San Francisco.
Shambulio la kwanza la bomu lilitokea mnamo Agosti 2003, nje ya Kituo cha Sayansi cha Chiron huko Emeryville, California.
Bomu la pili lilipatikana katika eneo hilo lakini lililipuka kabla halijateguliwa.
Shirika hilo lilisema iliibua uwezekano wa kifaa hicho kupandwa mahsusi ili kulenga ambao wangejitokeza wa kwanza.
Chini ya mwezi mmoja baadaye, mnamo Septemba 2003, bomu lililipuka nje ya shirika la bidhaa za lishe lililoko Pleasanton, California.
Alikua "gaidi wa ndani" wa kwanza kuongezwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa zaidi na shirika hilo, lililoundwa na Rais wa wakati huo George W Bush mnamo Oktoba 2001 kufuatia shambulio la 9/11.
Nani wapo katika orodha ya wanaosakwa zaidi na FBI?

Chanzo cha picha, Getty Images
Bw San Diego alionekana kwenye orodha hiyo pamoja na Osama Bin Laden, ambaye inaaminika aliongoza mashambulizi ya 9/11, na aliuawa na majeshi ya Marekani nchini Pakistan mwaka 2011.
Michael J Heimbach, mkurugenzi msaidizi wa FBI kutoka kitengo cha kukabiliana na ugaidi, alisema mshukiwa alifanya "vitendo vya kigaidi vilivyopangwa na pengine vilivyokusudia kuua".
Kwa mujibu wa ripoti, shirika hilo lilimwona mara ya mwisho mnamo 2003 wakati maafisa wa FBI walipokuwa karibu,katikati mwa jiji la San Francisco.
"Aliegesha gari lake, akashuka kwenye gari lake na kuanza kutembea barabarani na, kama sijakosea, aliingia kwenye kituo cha garimoshi cha Bart na hiyo ilikuwa mara ya mwisho kumwona," afisa wa FBI David Johnson alisema mnamo 2013.