Nilitazama ponografia asubuhi, mchana na usiku'
Nilitazama ponografia asubuhi, mchana na usiku'
Shaun Flores alikuwa na umri wa miaka 11 alipoanza kutazama ponografia, baada ya kutambulishwa aina hizo za video na rafiki yake.
"Nilivutiwa mara moja," kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 sasa anasema.
"Nilihisi, msisimo nikasema wow, ni kitu gani hiki ambacho watu wakifanya wanaonekana kama wana wakati wa mzuri wa maisha yao."
Udadisi wa Shaun haraka ukabadilika na kuwa kitu ambacho alikiona ni vigumu kukiacha.
Anaeleza kuwa alitazama ponografia asubuhi, mchana na usiku, akisema ikawa "kawaida kama kupiga mswaki".
Ingawa sio kila mtu anayetazama ponografia ataendeleza uhusiano usiofaa nayo, Shaun hayuko peke yake katika tabia hii ya kutazama ponografia.
Ripoti ya shirika la Ofcom ya Online Nation 2024 inasema 29% ya watu wazima wa Uingereza walitazama ponografia mtandaoni Mei 2024.
Zaidi ya hayo, utafiti mpya kutoka kituo cha matibabu ya watu walioathiriwa, UKAT, unaonyesha kuwa mamilioni ya Waingereza wanatazama ponografia mara kwa mara, huku milioni 1.8 wakitazama kila siku, au mara kadhaa kwa siku.
Kulingana na wanaotibu uraibu huo, watu wengi zaidi wanatafuta usaidizi kwa utumiaji wa ponografia wenye shida.
'Mara tu unapoanza ni ngumu sana kuacha'
Lee Fernandes, mtaalamu wa tiba katika Kundi la UKAT, pia anasema idadi ya watu wanaowatibu kwa matumizi mabaya ya ponografia imeongezeka "kwa kiasi kikubwa" katika miaka ya hivi karibuni.
Sasa wanapokea maswali mengi kwa usaidizi kutoka kwa watu wanaopambana na utumiaji wao wa ponografia kila siku. Kabla ya 2020, ilikuwa ni swali moja au mbili kwa wiki
Fernandes anaeleza kuwa maendeleo ya teknolojia na upatikanaji rahisi wa ponografia unarahisisha watu wa rika zote kufikia maudhui ya ngono mtandaoni. Anaamini yake inachangia ongezeko la watu wanaotafuta msaada ambao amepata.