Skip to main content

Tetesi za soka Ulaya: Juventus kumnasa Liam Delap?

 

Tetesi za soka Ulaya: Juventus kumnasa Liam Delap?

Liam Delap

Chanzo cha picha, Getty Images

Juventus wanafikiria kumnunua Liam Delap wa Ipswich na wametuma maskauti kumtazama mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21, ambaye pia anazivutia Chelsea na Manchester United. (Mirror)

Klabu hiyo ya Italia pia inatazamia kumnunua mshambuliaji wa Manchester United kutoka Uholanzi Joshua Zirkzee, 23 kwa mkopo. (Gazzetta dello Sport)

Paris St-Germain wanavutiwa na mshambuliaji wa Chelsea wa Ufaransa Christopher Nkunku mwenye umri wa miaka 27 na huenda wakamtoa mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 25, kwa kubadilishana naye. (TBR Football)


christopher nkunku

Chanzo cha picha, Getty Images

Winga wa Liverpool Federico Chiesa, 27, ni chaguo ambalo Napoli inafikiria kuchukua nafasi ya Khvicha Kvaratskhelia ikiwa mshambuliaji huyo wa Georgia hatatia saini mkataba mpya katika klabu hiyo ya Serie A. (Il Napolista)

Aston Villa huenda wakamkumbuka Louie Barry kutoka kwa mkopo Stockport mwezi Januari na kumpeleka kwa mkopo katika klabu ya Championship, huku Sheffield Wednesday na Middlesbrough wakiongoza mbio za kumsaka mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21. (Star)

Manchester United hawana uwezekano wa kumpa Christian Eriksen mkataba mpya, huku mkataba wa sasa wa kiungo huyo wa kati wa Denmark mwenye umri wa miaka 32 ukikamilika mwishoni mwa msimu. (Florian Plettenberg)

Christian Eriksen

Chanzo cha picha, Getty Images

Crystal Palace ni miongoni mwa vilabu vingi vya Ulaya vinavyohitaji kumnunua beki wa pembeni wa Lecce raia wa Denmark Patrick Dorgu. (CaughtOffside)

Manchester United imemruhusu mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, kuondoka kwa uhamisho. (Fichajes - kwa Kihispania)

Everton hawana uwezekano wa kukamilisha mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Roma,Bryan Cristante, 29, wakati wa dirisha la usajili la Januari. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 28, anaweza kuwa njiani kuondoka Real Madrid huku Real Betis wakiwa na nia ya kumrejesha mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal katika klabu hiyo. (Fichajes)

Popular posts from this blog

Vita vya Urusi na Ukraine: Matukio matano muhimu ya faida na hasara kwa Putin 2024

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Wanawake 100 wa BBC 2024: Ni nani yuko kwenye orodha mwaka huu?