Tetesi za soka Ulaya: Real wamtaka Alexander-Arnold

 

Tetesi za soka Ulaya: Real wamtaka Alexander-Arnold

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Trent Alexander-Arnold

Real Madrid wameifahamisha Liverpool kuhusu nia yao ya kutaka kumsajili beki wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26. (TalkSport)

Kocha mpya wa Manchester United Ruben Amorim ameazimia kufanya kazi na wachezaji wake wa sasa na hajatuma ombi kwa uongozi wa klabu kuhusu usajili wowote wa Januari. (Sky Sports)


g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lutsharel Geertruida

Tottenham wana nia ya kumsajili beki wa kulia wa RB Leipzig Mholanzi Lutsharel Geertruida, mweney umri wa miaka 24, kama kiungo mbadala wa Pedro Porro, mwenye umri wa miaka 25, ambaye analengwa na Real Madrid . (Caught Offside)

Mshambuliaji wa Ipswich Town mwenye umri wa miaka 21, Liam Delap anavutiwa na vilabu kadhaa vya Ligi ya Primia. (Athletic - subscription required)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Cunha

Manchester United na Tottenham zinaendelea kuhusishwa na taarifa za kutaka kumnunua Cunha lakini meneja wa Wolves Gary O'Neil amekataa kuondoka Januari. (MEN)

Aston Villa wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa kati wa Werner Bremen na Austria Romano Schmid, mwenye umri wa miaka 24. (Football Insider)


g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Patrick Dorgu

Chelsea wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa Denmark Patrick Dorgu, 20, kutoka Lecce , ambaye anaweza kuhitaji malipo ya takriban £50m. (Caught Offside)

Wolves itampatia kandarasi mpya yenye faida kubwa mshambuliaji wa Brazil ambaye yuko katika hali nzuri kimchezo Matheus Cunha, ambaye ana umri wa miaka 25 (Telegraph - subscription required)

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dominic Calvert-Lewin

Everton wanataka kuendelea kuwa na mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin, mwenye umri wa miaka 27, Januari licha ya uvumi kuhusu mustakabali wake. (Football Insider)

Tottenham, Crystal Palace na Nottingham Forest pia wanavutiwa na Dorgu. (TBR).

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Viktor Gyokeres

Hatua ya Arsenal ya kutaka mshambuliaji mpya imepata pigo kwa Viktor Gyokeres, 26, anayetaka kumfuata meneja wa zamani wa Sporting Lisbon Ruben Amorim kwenda Manchester United. (Football.London)

Beki wa Crystal Palace, 24, Muingereza, Marc Guehi, anatamani kujiunga tena na Chelsea, wakati Newcastle pia bado wanavutiwa na beki huyo wa kati. (TeamTalks

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Brazil Douglas Luiz

Manchester City na Manchester United wamepewa fursa ya kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 26, na kiungo wa kati wa Italia na Juventus Fagioli, 23, . (Gazzetta dello Sport - In Itali)

Meneja wa Chelsea Enzo Maresca amekanusha kuwa Christopher Nkunku anauzwa, licha ya fowadi huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27 kuwa na muda mfupi wa kucheza. (Times - Subnscription Required)

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China