Waasi wa Syria wanadhibiti nusu ya Aleppo, waangalizi wasema

 

Waasi wa Syria wanadhibiti nusu ya Aleppo, waangalizi wasema

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Vikosi vya waasi nchini Syria vimechukua udhibiti wa "nusu" ya mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, Aleppo, kwa mujibu wa shirika la waangalizi wa haki za binadamu wa Syria -Syrian Observatory for Human Rights (SOHR) lenye makao yake nchini Uingereza.

SOHR ilisema watu 277 ikiwa ni pamoja na zaidi ya raia 20 wameuawa tangu mashambulizi kuanza siku ya Jumatano.

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waasi wanaendesha gari kwenye barabara kuu ya kimataifa ya M5, njia ya kuelekea Aleppo, Syria

Mashambulizi hayo ni makubwa zaidi dhidi ya serikali ya Syria kuwahi kushuhudiwa kwa miaka mingi na ni mara ya kwanza kwa waasi wanaopigana na vikosi vya Rais Bashar al-Assad kufika Aleppo tangu kulazimishwa kuondoka mjini humo na jeshi mwaka 2016.

Uwanja wa ndege wa Aleppo na barabara zote zinazoingia mjini zimefungwa, vyanzo vya kijeshi vililiambia shirika la habari la Reuters.

Popular posts from this blog

Jeshi la Wanamaji la Marekani limesema linakabiliwa na vita 'kali zaidi' tangu Vita vya Pili vya Dunia dhidi ya Wayemeni

Putin asaini mkataba wa kituo cha Mwezi na China