Ahadi ya Al-Joulani ya kushirikisha Wasyria wote katika uendeshaji nchi imethibiti kuwa ni uongo
Kwa kuanza kwa wimbi la timuatimua ya maafisa wa jamii ya Maalawi katika wizara za serikali ya Syria, imethibiti kuwa ahadi alizokuwa ametoa Abu Muhammad Al-Jolani za kutotengwa tabaka lolote la jamii ya Wasyria katika uendeshaji nchi ni za uongo.
Al-Jolani, ambaye ni kiongozi wa kundi la kigaidi la Tahrir
al-Sham, alikuwa hapo awali amedai kwamba, hana nia ya kulitenga kundi
au tabaka lolote la Wasyria, lakini viongozi wa jamii ya Maalawi
wamewekwa kando katika orodha mpya iliyotolewa ya majina ya maafisa 34
wa nchi hiyo ambayo imeandaliwa kwa kutumia vigezo na utashi wa kidini
na kimadhehebu.
Duru za ndani ya Syria zimetangaza kuwa al-Jolani na wahusika walio
chini ya uongozi wake wanatekeleza sera ya kuhakikisha hakuna afisa
yeyote wa jamii ya Maalawi anayesalia katika taasisi ya serikali.
Kwa mujibu wa duru hizo, sera hiyo ya al-Jolani inatekelezwa kimyakimya na kwa siri.
Itakumbukwa kuwa, kuanzia Novemba 27, 2024, wapinzani wabeba silaha
nchini Syria walianzisha operesheni za kijeshi katika maeneo ya
kaskazini-magharibi, magharibi na kusini magharibi mwa mji wa Aleppo kwa
lengo la kumuondoa madarakani Bashar al-Assad; na hatimaye baada ya
siku 11, mnamo Desemba 8, walitangaza habari ya kulidhibiti jiji la
Damascus na kuondoka Assad nchini humo.../
Tags