Hii inaweza kuwa ajali mbaya zaidi ya ndege nchini Korea Kusini

 


Jean Mackenzie

Mwanahabari wa Seoul

Ajali hii si ya kawaida kwa Korea Kusini, ambayo imekuwa na rekodi nzuri ya usalama wa ndege katika miaka ya hivi karibuni.

Ikiwa idadi ya vifo itathibitishwa, hii itakuwa ajali mbaya zaidi ya ndege kuwahi kutokea katika ardhi ya Korea Kusini.

Inaonekana pia kuwa ajali mbaya pekee ambayo Jeju Air imepata katika historia yake ya karibu miaka 20.

Jeju Air ndilo shirika maarufu la ndege la bei nafuu nchini Korea Kusini, lenye safari nyingi za ndege katika eneo lote la Asia.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo alisema katika mkutano na wanahabari hapo awali shirika hilo la ndege halikuwa na historia ya ajali. Aliomba msamaha kwa familia za waathiriwa.