India: Waziri mkuu wa wa zamani Singh azikwa
India siku ya Jumamosi imetoa heshima za mwisho kwa Waziri Mkuu wa zamani Manmohan Singh, anayejulikana kwa mageuzi yake ya kiuchumi yaliyoifanya nchi hiyo kuwa kubwa duniani.
Manmohan Singh ambaye aliyefariki siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 92, anasifiwa kwa kusimamia katika muhula wake wa kwanza ukuaji wa uchumi wa nchi yake, ambayo sasa ni ya tatu kwa uchumi mkubwa duniani. Manmohan Singh, aliongoza India kutoka mwaka 2004 hadi mwaka 2014,
Baada ya heshima ya mwisho kwa makao makuu ya chama chake, Indian National Congress, jeneza lake lililofunikwa kwa maua lilibebwa kupitia New Delhi, likisindikizwa na vikosi vya usalama.
Rais Draupadi Murmu na Waziri Mkuu Narendra Modi wamehudhuria mazishi hayo katika mji mkuu, pamoja na maafisa wakuu wa kiraia na kijeshi.
Mfalme wa Bhutan, Jigme Khesar Namgyel Wangchuck, pia alikuwepo kwenye sherehe hiyo, ambapo heshima za kijeshi zilitolewa kwa Waziri Mkuu kwa risasi za mizinga, kabla ya kuchomwa kwake.
Kipindi cha siku saba cha maombolezo ya kitaifa kilianza rasmi siku ya Alhamisi na kinaendelea hadi siku ya Jumatano.
Narendra Modi ametoa pongezi kwa "mmoja wa viongozi wakuu" ambao India inawafahamu, huku Rais Murmu akisifu "huduma inayotolewa kwa taifa" na "unyenyekevu wake wa hali ya juu".
Kiongozi wa upinzani Rahul Gandhi, ambaye amesali pamoja na familia ya marehemu, amesema amepoteza "mshauri na kiongozi", ambaye aliongoza nchi "kwa hekima kubwa na uadilifu".
Manmohan Singh aliyezaliwa mwaka wa 1932 huko Gah katika nchi ambayo sasa inaitwa Pakistan, alipata ufadhili wa masomo ya uchumi katika Cambridge na Oxford, ili kuondoa umaskini nchini mwake.
Alikuwa ameshikilia nyadhifa kadhaa za juu katika utumishi wa umma na alifanya kazi kwa mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa mataifa, lakini hakuwahi kushika wadhifa wa kuchaguliwa kabla ya kuwa mkuu wa serikali.
Gavana wa Benki Kuu ya nchi hiyo, aliombwa mwaka 1991 kuiondoa India katika mzozo mbaya zaidi wa kifedha katika historia yake ya kisasa.
Wakati wa muhula wake wa kwanza, uchumi wa India ulikua 9% kila mwaka, na kuifanya nchi hiyo kuwa ya kimataifa ambayo ilikuwa ikitafuta kwa muda mrefu.
Kupungua kwa ukuaji katika miaka iliyofuata, hata hivyo, kuliharibu muhula wake wa pili.
Akijulikana kama "Bwana Msafi", aliona taswira yake ikichafuliwa wakati wa miaka kumi madarakani baada ya kufichuliwa kwa msururu wa kesi za ufisadi.
Bwana Singh amekuwa mkosoaji mkubwa wa sera za kiuchumi za Waziri Mkuu Modi, pia akionya juu ya hatari zinazoletwa na kuongezeka kwa mivutano ya kijamii kwa demokrasia ya India.
Alitia muhuri mkataba wa kihistoria wa nyuklia na Marekani ambao alisema utasaidia India kukidhi mahitaji yake ya nishati yanayoongezeka.
Rais wa Marekani Joe Biden amemsifu "mwanasiasa wa kweli" kwa "kuanzisha maendeleo ambayo hayajawahi kutokea ambayo yataendelea kuimarisha mataifa yetu, na ulimwengu, kwa vizazi vijavyo".