Iran: Marekani inalenga kuwapora Waislamu, haitafanikiwa chochote nchini Syria

 

  • Iran: Marekani inalenga kuwapora Waislamu, haitafanikiwa chochote nchini Syria

Jeshi la Iran linasema kutimuliwa kwa Rais Bashar al-Assad wa Syria na wanamgambo wanaoungwa mkono na mataifa ya kigeni ni njama ya Wamarekani na Wazayuni, lakini Marekani haitafanikiwa lolote katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Kamandi Kuu ya Majeshi ya Iran imesema katika taarifa: "Matukio ya hivi karibuni katika eneo hilo, bila kusahau matukio ya Syria, yanaonyesha kuendelea kwa uovu, ukosefu wa usalama na kina cha uadui wa kiburi cha ulimwengu, kinachoongozwa na uovu mkubwa ya Marekani ya uhalifu, dhidi ya mataifa yanayotafuta uhuru."

Taarifa hiyo imebainisha kuwa: “Pasiwe na shaka kwamba yaliyotokea Syria ni zao la njama ya pamoja ya Marekani na Kizayuni. Ni dhahiri kwamba mfumo wa kivita unaoongozwa na Marekani katika eneo la Asia Magharibi unalenga kufikia malengo yake maovu, ikiwa ni pamoja na kupora rasilimali na kuwafanya Waislamu kuwa watumwa."

Kamandi Kuu ya Majeshi ya Iran imesema imesisitiza utayari wa Jamhuri ya Kiislamu kutoa jibu kali na thabiti kwa vitisho na vitendo vyovyote vya uchokozi dhidi ya nchi.

Taarifa hiyo imesema uistikbari wa kimataifa unaoongozwa na Marekani potovu na kusaidiwa na utawala mbovu na unaoua watoto wa Kizayuni, umefanya kila uwezalo katika kipindi cha miaka mingi kukabiliana na Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979 lakini njama hizo zimefeli.

Taarifa hiyo imesema kwamba uistikbari wa kimataifa unaichukulia Jamhuri ya Kiislamu kuwa kikwazo kikubwa zaidi kwa ukandamizaji na jinai yake na kuongeza kuwa: "Kwa hiyo, uistikbari unajaribu kutumia uwezo wote wa kimataifa na kieneo ili kuondokana na kikwazo hiki."

Jeshi la Iran linasema: “Hata hivyo, iwapo uistikbari utachunguza yaliyojiri huku nyumba basi utafahamu kwamba, kkama ilivyokuwa hapo awali, njama zao zote zitasambaratishwa na  taifa shujaa la Iran ya Kiislamu, na kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, hawatapata chochote huko Syria pia."