Iran: Shambulio la Israeli katika Hospitali ya Kamal Adwan ni 'uhalifu mbaya wa kivita'

 

  • Iran: Shambulio la Israeli katika Hospitali ya Kamal Adwan ni 'uhalifu mbaya wa kivita'

Iran imekemea shambulio la kikatili la utawala wa Israel kwenye Hospitali ya Kamal Adwan katika eneo la kaskazini mwa Gaza kama “uhalifu mbaya wa kivita” na sehemu ya mauaji ya kimbari yanayoendelea kwenye ardhi za Palestina zilizokaliwa kwa mabavu na kusema kimya cha taasisi muhimu za kimataifa kuhusu suala hilo kama “hakikubaliki.”

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Esmaeil Baghaei, katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, alilaani uvamizi wa kikatili wa Israeli kwenye hospitali hiyo na uharibifu mkubwa wa sehemu nyingi zake kama mfano wa hivi karibuni wa uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, na ukiukaji wa wazi wa sheria na kanuni za kimataifa.

Alisema kwamba ukatili huu ulitekelezwa kwa lengo la kuharibu kabisa mfumo wa huduma za afya katika Gaza, na kuwanyima watoto, wanawake, watu waliojeruhiwa na wagonjwa ufikiaji wa huduma za matibabu za hali ya chini.

Baghaei alisisitiza kwamba Hospitali ya Kamal Adwan ilikuwa miongoni mwa vituo vya matibabu vinavyofanya kazi vya mwisho kaskazini mwa Gaza, akitaja shambulio la kijeshi la Israeli kwenye hospitali hiyo na kuwahamisha kwa nguvu wagonjwa na wahudumu wa afya kama “uhalifu mbaya wa kivita na sehemu ya mauaji makubwa yanayoendelea katika Palestina iliyokaliwa kwa mabavu.”

Mwanadiplomasia huyo mwandamizi wa Iran amelaumu alilaumu kimya cha taasisi husika za kimataifa kuhusiana na uhalifu huo na kisema kimya kama hicho “siyo ya haki,.”

Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), uvamizi wa jeshi la Israeli kwenye Hospitali ya Kamal Adwan umesababisha kufungwa kwa kituo hicho cha afya cha mwisho kinachofanya kazi kaskazini mwa Gaza na idara kuu ziliharibiwa na moto wakati wa uvamizi.