Je kuna faida ya kula manjano na viungo vingine?

Chanzo cha picha, Getty Images
Pilipili, manjano na viungo vingine zinadaiwa kuwa na umuhimu katika afya na pia kuboresha “kingamaradhi .” Je viungo vinaongeza virutubisho kwa vyakula au kutukinga na maradhi?
Viungo kama manjano, pilipili, na tangawizi vimekuwa sehemu muhimu ya lishe yetu kwa maelfu ya miaka. Hivi karibuni, viungo hivi vimekuwa vikitangazwa kama vyakula vyenye faida za kiafya, na wengi wanadai kwamba vinaweza kuimarisha mfumo wa kinga na kutibu magonjwa.
Inasemekana Hillary Clinton alikuwa akipenda kula pilipili moja kwa siku akiwa katika msururu wa kampeini 2016 kama njia moja ya kujikinga na maradhi.
Manjano, imekuwa ikitumiwa Asia kwa miongo, na imeanza kutumiwa katika kupika kahawa almaarufu golden lattes.- na wakati wa uviko 19, iliaminika manjano yanaimarisha mfumo wa kinga mwilini na kukuepushia magonjwa.
Hayo yakijiri, pilipili kichaa bado haijapata umaarufu baada ya utaratibu wa mlo wa kupotosha wa Msanii Beyonce ya mwaka 2013 ambayo iliendekeza kutumia mchanganyiko wa pilipili kichaa kioevu ya maple, limao na maji ili kupunguza uzito.
Lakini je, viungo vina faida yoyote za kiafya kwa chakula chetu au vinaweza kutusaidia kujikinga na magonjwa?
Na je, baadhi yao vinaweza kutuletea madhara?
Faida za kiafya za pilipili
Pilipili ni mojawapo ya viungo vinavyotumika sana na inavyojulikana duniani kote.
Tafiti nyingi zimechunguza athari zake kwenye afya yetu na matokeo yamekuwa na mchanganyiko wa faida na madhara.

Chanzo cha picha, Getty Images
Capsaicin ni kiungo kikuu cha ufanisi katika pilipili. Tunapokula pilipili, molekuli za capsaicin huchangamana na vipokezi vya joto mwilini mwetu na kutuma ishara kwenda kwenye ubongo kutoa hisia ya joto.
Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa pilipili kichaa inaweza kuongeza muda wa kuishi.
Utafiti wa 2019 ulionyesha kuwa wale wanaokula chakula kilicho na pilipili mara 4 kwa wiki wanakuwa na hatari ndogo ya kufa kuliko wale wasio kula pilipili.
Lakini faida hizi huenda zikajitokeza polepole kwa muda mrefu.
Na mwaka 2015, watafiti kutoka uchina ambao walitathmini utumizi wa pilipili na afya ya raia wa China laki unusu, waligundua kuwa kula pilipili kunahusishwa na hatari ndogo ya kifo.
Wale ambao walitumia vyakula vya viungo kila siku walikuwa na hatari ya chini ya asilimia 14 ya kifo kuliko wale waliokula vyakula vya viungo chini ya mara moja kwa wiki.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Tafiti nyingi kuu zimeonyesha kwamba pilipili inaweza kusaidia kupunguza hatari ya kifo, hasa kutokana na magonjwa kama saratani, magonjwa ya moyo, na magonjwa ya kupumua,” Anasema mtafiti Lu Qi,Profesa wa lishe bora katika kitivo cha afya ya umma chuo kikuu cha Harvard’s.
Hata hivyo, haina maana kuwa kubugia pilipili nyingi kutalinda afya yako – au magonjwa yakupumua katika kipindi kifupi.
Ni muhimu kukumbuka kwamba utafiti wa China ulifuatilia watu kwa wastani wa miaka saba. Hata kama pilipili ilikuwa na athari ya kinga kwa afya ya walioshiriki kwa utafiti, waliokula pilipili walikuwa na afya bora tangu awali, kinga ilijijenga polepole kwa muda na si ndani ya wiki au miezi michache.
Qi alijaribu kutenganisha athari za ulaji wa pilipili na mambo mengine kwa kudhibiti umri, jinsia, kiwango cha elimu, hali ya ndoa, mlo na mtindo wa maisha, ikiwa ni pamoja na ubugiaji wa pombe, uvutaji sigara, na shughuli za kimwili.
Anasema kuwa hatari ndogo ya magonjwa inayohusiana na ulaji wa pilipili huenda inatokana na capsaicin.
“Viambato fulani katika vyakula vya pilipili, kama capsaicin, vimeonekana kuboresha hali ya uvunjaji vunjaji wa kemikali mwilini, kama vile viwango vya mafuta mwilini na uvimbe uchungu na haya yanaweza kuchangia katika matokeo tuliyoyaona kwenye utafiti wetu,” anasema Qi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pia kuna tafiti kadhaa zimeonyesha kuwa capsaicin inawaongeza nguvu tunayoyeyusha na kupunguza hamu ya kula.
Zumin Shi, profesa msaidizi katika Idara ya Lishe ya Binadamu ya Chuo Kikuu cha Qatar, amegundua kuwa ulaji wa pilipili unahusiana na hatari ndogo ya unene kupita kiasi na ni faida kwa shinikizo la damu la juu.
Alipofanya utafiti kuhusu athari za pilipili kwenye utendaji wa ubongo, alitarajia kuona matokeo mazuri.
Lakini alipopima utendaji wa ubongo wa watu wazima wa China kulinganisha na ulaji wao wa pilipili, aligundua kuwa wale waliokula pilipili zaidi walikuwa na utendaji duni wa ubongo.
Athari hii ilionekana zaidi kwa kumbukumbu: ulaji wa pilipili zaidi ya gramu 50 kwa siku ulijulikana kuwa na hatari mara mbili ya kumbukumbu duni iliyoripotiwa.
Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa taarifa zinazoripotiwa na mtu binafsi mara nyingi haziaminiki.
Muwasho unapokula pilipili imewavutia wanasayansi kwa muda mrefu. Hisia ya moto inayosikika unapokula pilipili imewavutia wanasayansi kwa muda mrefu.
Inatufunulia pia kwanini pilipili inaweza kuwa na uhusiano na upungufu wa uwezo wa kiakili: hisia hii ni matokeo ya mimea kujiendeleza ili kujilinda dhidi ya magonjwa na wadudu.
"Wakati mimea mingine inabadilika na kuwa chungu au msisimko ili kujilinda na wanyama waharibifu, ni bora pia ikiwa mmea unaweza kuwa na sumu,” anasema Kirsten Brandt, mhadhiri mkuu katika Kituo cha Utafiti wa Lishe ya Binadamu, Taasisi ya Sayansi za Afya ya Idadi ya Watu, Chuo Kikuu cha Newcastle, Uingereza.
Hata hivyo viambato vina athari ndogo kwa binadamu ukilinganisha na wadudu.
"Sumu kidogo inaweza kuwa nzuri kama vile kahawa, ambayo huchochea metaboliki yetu ili tuwe na nguvu zaidi", anasema mtaalam.
Lakini ukizidisha sumu ni hatari kwa binadamu”.
Kwa upande mwingine, hata kama kiambato fulani katika kiungo kinaweza kuwa na faida, mara nyingi hatuli kiasi cha kutosha ili kuona athari yoyote kubwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Manufaa ya kiafya ya Manjano
Kiungo maarufu kinachojulikana kwa manufaa yake ya afya ya binadamu ni manjano ambayo inahusishwa sana na curcumin, molekuli ndogo inayopatikana kwenye Manjano.
Curcumin hutumika sana katika tiba mbadala kutibu maumivu, msongo wa mawazo, na hali nyingine mbalimbali za kiafya.
Watafiti wengi wanaamini kwamba manufaa ya afya ya viungo yanaweza kutokana na chakula tunachoambatanisha nao.
Hata hivyo, ushahidi wa kuthibitisha kuwa manjano inafaidi afya kwa wingi.
Ingawa tafiti nyingi zimeonyesha kwamba curcumin ina athari za kupambana na saratani katika maabara, mazingira ya maabara ni tofauti sana na mwili wa binadamu.
Watafiti wanasema kuwa uwezo wa mwili kunyonya curcumin ni wa chini sana kwa kiasi cha kawaida cha chakula, hivyo hakiwezi kutoa manufaa makubwa kwa afya.
Hali hii inaweza pia kuwa kwa viungo vingine. Hata hivyo, baadhi ya watafiti wamechunguza manufaa ya virutubisho vya viungo vinavyokuwa na dozi kubwa ya viungo fulani na kugundua matokeo yenye matumaini.
Kwa mfano, utafiti wa mwaka 2023 uligundua kuwa kuchukua virutubisho vya tangawizi kila siku kunaweza kusaidia kudhibiti maumivu kwa watu wenye magonjwa ya autoimmune kama vile lupus na maumivu ya mifupa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hamu yetu ya kisasa kwa viungo inatufanya kuwa na mtazamo wa zama za kati kuliko miaka 50 iliyopita - wakati kulikuwa na uzio kati ya tiba za kisasa kama vile antibiotiki na tiba za kishirikina za zamani ambazo hazikuwa na matokeo.”
Kathryn Nelson, mtaalamu wa zamani wa utafiti katika Taasisi ya Ugunduzi na Maendeleo ya Dawa ya Chuo Kikuu cha Minnesota, aliona umuhimu wa kuchunguza curcumin baada ya kukutana mara kwa mara na madai ya kiafya yanayohusiana nayo.
"Tafiti zinaweza kuzidisha athari kwa seli zilizokuwa kwa maabara kwa kuongeza viambato ili kuona ni kipi kitafanyika kwa seli hizo,” anasema Kathryn.
Lakini aligunduwa kuwa curcumin ni molekuli ‘mbaya” kwa ajili ya dawa, kwa sababu haipatikani kwa urahisi kwa mwili baada ya kumeza.
Haingii kwa urahisi kwenye utumbo mdogo, na muundo wake unaweza kubadilika inapoungana na protini kwenye utumbo mdogo na mkubwa. Hivyo, haifanyi kazi sana.

Chanzo cha picha, Getty Images
Watafiti wengi wanaamini kwamba manufaa ya kiafya ya viungo yanatokana na kile tunachokula pamoja navyo.
Kwa mfano, kuna tabia ya kutumia viungo mbadala vya chumvi, anasema Lipi Roy, profesa msaidizi wa kliniki katika kituo cha afya cha NYU Langone huko New York.
“Viungo hufanya chakula kuwa kitamu na chenye ladha nzuri, na vinaweza kuwa mbadala bora wa chumvi,” anasema.
Kwa kweli, mwaka jana, watafiti walithibitisha kuwa kubadilisha chumvi na mafuta yaliyojaa viungo kunaweza kufanya vyakula maarufu kuwa na ladha nzuri kama vilivyowekwa chumvi.

Chanzo cha picha, Getty Images