Je, Urusi itawaachilia maelfu ya wanajeshi wa Ukraine kwa mwaka mpya?

Afisa mmoja wa Ukraine ameiambia BBC wanatumai mabadilishano ya wafungwa ya Mwaka Mpya na Urusi yatafanyika "siku yoyote," ingawa mipango inaweza kuafikiwa dakika za mwisho.
Petro Yatsenko, kutoka Makao Makuu ya Ukraine kwa ajili ya Matibabu ya Wafungwa wa Vita, alisema mazungumzo na Moscow kuhusu kubadilishana wafungwa yamekuwa magumu zaidi katika miezi ya hivi karibuni tangu majeshi ya Urusi yaanze kufanya kupiga hatua kubwa katika mstari wa mbele.
Kulikuwa na mabadilishano 10 pekee mwaka 2024, ikiwa ni idadi ya chini kabisa tangu uvamizi wa wa Urusi nchini Ukraine uanze.
Ukraine haichapishi idadi ya wafungwa wa vita wanaoshikiliwa na Urusi, lakini jumla inadhaniwa kuwa zaidi ya 8,000.
Urusi imepata mafanikio makubwa katika medani ya vita mwaka huu, na kuzua hofu kwamba idadi ya raia wa Ukraine wanaokamatwa inaongezeka.