Jeshi la IRGC lasema liko tayari kulinda usalama wa Iran

 

  • Jeshi la IRGC lasema liko tayari kulinda usalama wa Iran

Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limeeleza utayari wake kamili wa kulinda usalama wa Iran na kukabiliana na njama za adui anayelenga kuleta machafuko na uchochezi nchini.

Katika taarifa iliyotolewa Jumapili, IRGC iliangazia kumbukumbu ya maandamano ya kitaifa ya kuunga mkono serikali yaliyofanyika mwaka a 2009 katika tarehe tisa ya mwezi wa Dey wa kalenda ya Kiajemi, ambayo ni sawa na Desemba 30.

IRGC imetaja Hamasa ya Dey 9 kama tukio la "utukufu na kuamua hatma" ambalo lilishangaza "mtandao wa uovu na jinai wa wahaini wanaopata himaya ya Marekani na Wazayuni".

Mnamo Desemba 30, 2009, mamilioni ya Wairani walikusanyika katika mji mkuu Tehran na miji mingine kumaliza miezi kadhaa ya ghasia za baada ya uchaguzi na kuonyesha utiifu wao kwa serikali ya Kiislamu.

Machafuko yaliyoungwa mkono na nchi za kigeni yalipangwa na Mehdi Karroubi na Mir Hossein Musavi, wagombea wawili walioshindwa katika uchaguzi wa urais, wakidai kuwa kulikuwepo na wizi wa kura..

Katika taarifa yake, IRGC ilisema Hamasa ya Dey 9 ilitoa majibu "madhubuti, makini na ya mwisho" kwa uchochezi uliotokana na uchaguzi wa urais wa Juni 2009.

IRGC pia imebainisha kwa kushirikiana na jeshi la kujitolea linalojulikana kama Basij liko tayari kulinda usalama wa kitaifa na amani ya Iran na kukabiliana na mipango ya adui ya kusababisha machafuko, ukosefu wa usalama na uchochezi nchini.