Maher al-Assad: "Mlinzi wa Familia" na "Mchinjaji wa Daraa", ni nani?

 

Maher al-Assad: "Mlinzi wa Familia" na "Mchinjaji wa Daraa", ni nani?

..

Chanzo cha picha, getty

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq ilikanusha kuwepo kwa Maher al-Assad, kaka wa Rais aliyepinduliwa nchini Syria Bashar al-Assad, ndani ya ardhi ya Iraq.

Katika taarifa ya msemaji wake iliyochapishwa na Shirika la Habari la Iraq, wizara hiyo ilivitaka vyombo vya habari "kutumia usahihi na tahadhari katika kusambaza habari kutoka vyanzo vyake rasmi," ikisisitiza kwamba kile kilichosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uwepo wa Maher al-Assad nchini Iraq. ilikuwa "isiyo ya kweli."

Tangu kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad wiki iliyopita, na kuondoka kwa rais aliyeondolewa madarakani na familia yake kwenda Moscow, kumekuwa na uvumi mwingi kuhusu hatima ya kaka yake Maher, ambaye anaelezwa kuwa "mlezi wa familia ya Assad. "Je tunafahamu nini kuhusu Maher al-Assad?

Baada ya kifo cha kaka yake Basil al-Assad katika ajali ya gari mnamo Januari 1994, kulikuwa na matarajio kwamba Maher anaweza kumrithi babake Hafez al-Assad kiti cha urais.

Chanzo cha picha, Getty

Maher Hafez al-Assad alizaliwa Damascus mnamo Desemba 8, 1967, na alikulia katika familia ya Assad iliyotawala Syria kwa miongo kadhaa.

Tangu utoto wake, Maher alijulikana kwa utu wake dhabiti na tabia ya uthubutu, lakini hakuonekana hadharani hadi mwishoni mwa miaka ya 1990.

Kwa mujibu wa ripoti, Assad anaishi karibu na ikulu ya rais huko Damascus, ni "mpanda farasi mwenye bidii" na anamiliki hifadhi ya farasi katika eneo la Yafour karibu na Damascus.

Mnamo 1999, Maher al-Assad aligonga vichwa vya habari baada ya ripoti kwamba alimpiga risasi shemeji yake, Assef Shawkat, kufuatia mzozo kati yao, na kumjeruhi Shawkat na kumhamishia katika hospitali ya kijeshi huko Ufaransa kwa matibabu.

Licha ya tukio hilo, Maher aliendelea kuimarisha nafasi yake ndani ya utawala wa Syria.

Mnamo Juni 2000, Maher alichaguliwa katika Kamati Kuu ya Chama cha Kisoshalisti cha Kiarabu cha Ba'ath, hatua ambayo iliimarishaa nafasi yake ndani ya utawala.

Baada ya kifo cha kaka yake Basil al-Assad katika ajali ya gari mnamo Januari 1994, kulikuwa na matarajio kwamba Maher angeweza kumrithi baba yake Hafez al-Assad madarakani, lakini tabia korofi ya Maher ilizuia hili, na Bashar alichaguliwa badala yake.

Gazeti la Uingereza la "The Telegraph" liliripoti kwamba "Wasyria wengi wanamwona Maher kama ujio mpya wa Rifaat" [ikimaanisha kaka wa marehemu Rais Hafez al-Assad]. Gazeti hilo liliripoti kwamba uhusiano wa Maher al-Assad na Bashar al-Assad "unatokana na mbinu ya vitendo" iliyoanzishwa na Hafez na Rifaat al-Assad.

Umoja wa Ulaya umemweka Maher al-Assad kwenye orodha ya maafisa wa Syria waliowekewa vikwazo, ukimtaja kama "msimamizi mkuu wa vurugu dhidi ya waandamanaji.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maandamano ya Syria dhidi ya serikali yalipoanza mwaka 2011, Maher al-Assad alichukua jukumu muhimu katika kukandamiza maandamano hayo.

Kama kamanda wa Kitengo cha 4 cha Kivita na jeshi la jamuhuri, alikuwa na mchango mkubwa katika kusimamia shughuli za kijeshi.

Kwa sababu hii, vyombo vya habari vilimtaja kama "Mchinjaji wa Daraa" baada ya kuhusika katika kukandamiza maandamano ya jiji mnamo Aprili 2011.

Jeshi la Republican, wakiongozwa na Maher al-Assad, ndio kitengo pekee katika jeshi la Syria kilichoruhusiwa kutumwa Damascus.

Mnamo Aprili mwaka huo huo, Rais wa Marekani Barack Obama alitoa amri ya kufungia mali ya Maher al-Assad nchini Marekani kutokana na "kuhusika kwake kuwakandamiza waandamanaji."

Umoja wa Ulaya pia ulimjumuisha katika orodha yake ya maafisa wa Syria waliowekewa vikwazo, ukimtaja kama "msimamizi mkuu wa ghasia dhidi ya waandamanaji."

Mnamo mwaka wa 2012, Taasisi ya kimataifa inayoshughulikia Migogoro lilichapisha ripoti ambayo baadhi ya wafuasi wa serikali ya Syria walimtaja Maher al-Assad kama "mtu hodari wa serikali."

..

Chanzo cha picha, Getty

Mwaka huo huo, kulikuwa na uvumi kwamba Maher al-Assad aliuawa au kujeruhiwa katika mlipuko uliomuua Assef Shawkat na viongozi wengine wakuu, lakini ripoti hizi zilikanushwa.

Pia alishutumiwa na Channel 2 ya Israel kwa kutoa amri ya kufanya mashambulizi ya silaha za kemikali katika eneo la Ghouta katika mashamba ya Damascus, ambayo yaliripotiwa kuua hadi watu 1,200 mwezi Agosti 2013.

Alipokuwa akiendelea kuwaamuru wanajeshi wa jamuhuri, Maher al-Assad alichukuliwa kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa zaidi katika jeshi la Syria, na vitengo vya kivita vya jeshi hilo vinasemekana kuwa vitengo tiifu zaidi vya serikali.

Mnamo Machi 2023, Marekani na Uingereza ziliweka vikwazo vya ziada kwa Maher al-Assad na washirika wake, pamoja na walanguzi wa dawa za kulevya, kwa madai ya kujihusisha na uuzaji haramu wa dawa na dawa za kulevya nchini Syria.

Wizara ya fedha ya Marekani ilishutumu Maher al-Assad na kwa kufadhili "mipango haramu ya kuzalisha mapato, kuanzia ulanguzi wa sigara na simu za mkononi hadi kuwezesha uzalishaji na dawa aina ya Captagon kimagendo.''

Mnamo Aprili 2023, Umoja wa Ulaya uliweka vikwazo kwa watu binafsi na makampuni yanayohusishwa na Maher al-Assad na kitengo cha masuala ya kivita kwa "kufanya uhalifu wa kivita, utesaji, na kuwezesha biashara haramu ya dawa za kulevya nchini Syria."

Utawala wa Assad ulitajwa kama "mhusika mkuu kuwezesha utoroshaji wa dawa aina ya Captagon hadi bandari za Ulaya."