Mji ambao kubeba silaha ni wajibu

- Author, Brandon Drenon
- Nafasi, BBC, Kennesaw, Georgia
Kennesaw, Georgia, ni mji mdogo wa Kusini Marekani ambao una mambo yote unayoweza kufikiria kuhusu miji ya kanda hii.
Harufu ya mikate inayookwa inanukia kutoka kwa tanuri mikate ya Honeysuckle Biscuits & Bakery, sauti ya treni inasikika kwa mbali, na wanandoa wapya wanaacha kadi walizoandika katika mkahawa wakishukuru kwa mazingira ya joto.
Lakini kuna jambo moja kuhusu Kennesaw ambalo linaweza kushangaza: sheria iliyopitishwa katika miaka ya 1980 inayowalazimisha wakazi wa mji huu kubeba silaha na bunduki.
"Sio kama utakavyobeba silaha kwenye eneo lako," anasema Derek Easterling, meya wa mji huu ambaye anahudumu muhula wake wa tatu na mwenye kusema kwamba yeye ni "mstaafu kutoka Jeshi la Wanamaji." "Hatuwezi kuvunja mlango wako na kusema, 'Onyesha silaha yako.'"
"Kwa kuhakikisha usalama na ustawi wa jumla wa mji na wakazi wake, kila mtu kwa familia anayeishi ndani ya mipaka ya mji atahitajika kumiliki bunduki pamoja na risasi zake," sheria ya Kennesaw inasema wazi.
Mtiririko wa sheria hii umetolewa na kutolazimishwa kwa wakazi wanaoishi na ulemavu na wale wenye ugonjwa wa kiakili, vilevile, kwa wale waliopatikana na hatia ya makosa ya jinai au wale ambao sheria inapingana na imani zao za kidini.
Meya Easterling ama viongozi wengi wa mji hawawezi kukumbuka kukamatwa au kufunguliwa mashtaka kwa kuikiuka Ibara II, Sehemu 34-21, ambayo ilianza kutekelezwa mwaka 1982.
Na hakuna mtu aliyeiambia BBC kuwa anaufahamu ni adhabu gani itolewayo kwa kuvunja sheria hii.
Hata hivyo, Meya anasisitiza, "Hii sio sheria ya kishawishi tu, na sipendi kufanya jambo lolote kwa ajili ya kujionyesha."
Kwa wengine, sheria hii ni chanzo cha fahari, kumbukumbu ya kujitolea kwa mji katika tamaduni za silaha.
Kwa wengine, ni chanzo cha aibu, ukurasa wa historia ambao wangependa kuugeuza.
Lakini hisia kuu kati ya wakazi wa mji kuhusu sheria ya kumiliki bunduki ni kwamba inafanya Kennesaw kuwa salama.
"Ni wahalifu ambao wanapaswa kuwa na tahadhari, kwa sababu wakivunja nyumba yako, hawawezi kujua kilicho ndani," wanasema wateja wanaokula pepperoni katika mkahawa wa kuuza mkate wa nyama ulioko mtaani.
Kwa mujibu wa Idara ya Polisi ya Kennesaw, hakukuwa na mauaji mwaka 2023, lakini kulikuwa na visa viwili vya kujitoa uhai vilivyohusisha kujipiga risasi.
Blake Weatherby, mchekeshaji katika Kanisa la Baptist la Kennesaw, ana maoni yake kuhusu kwanini viwango vya uhalifu wa vurugu vinaweza kuwa vya chini.
"Sio bunduki zinazoshusha uhalifu hapa Kennesaw, bali ni mtazamo," anasema Weatherby. "Iwe ni silaha, uma, ngumi, au viatu virefu, tunajilinda sisi wenyewe na majirani zetu."

Kulingana na Pat Ferris, aliyejiunga na Baraza la Mji la Kennesaw mwaka 1984, miaka miwili baada ya sheria hii kupitishwa, amedai kwamba kanuni hii iliandikwa "kama tamko la kisiasa kuliko kitu kingine chochote."
Baada ya Morton Grove, Illinois kuwa mji wa kwanza Marekani kupiga marufuku kumiliki silaha, Kennesaw ilikua mji wa kwanza kuwa na sheria inayolazimisha kumiliki silaha, jambo lililogonga vichwa vya habari vya kitaifa.
Makala moja ya mwaka 1982 katika gazeti la New York Times ilisema kwamba viongozi wa Kennesaw "waziwazi walifurahi" kupitisha sheria ya silaha, jambo ambalo haliwezi kusemwa kuhusu "wanazuoni wa uhalifu wa Yankee."
Pia, jarida la Penthouse liliripoti hali hii, likiwa na kichwa cha habari cha "Gun City USA: Mji wa Marekani ambapo ni kosa kutokuwa na Silaha" juu ya picha ya mrembo mwenye nywele za rangi ya dhahabu akiwa amevaa bikini.
Sheria za silaha kama hizi zimepitishwa angalau katika miji mitano mingine, ikiwemo Gun Barrel City, Texas, na Virgin, Utah.
Katika miaka 40 tangu sheria ya silaha ya Kennesaw ilipopitishwa, Ferris alisema kwamba kumbukumbu ya sheria hii imepungua sana katika fikra za wengi.
"Sijui ni wangapi wanajua kama kanuni hii bado ipo," anasema.

Mkulima wa bustani ya kanisa, Weatherby, alizaliwa mwaka ambao sheria za bunduki zilianza kutekelezwa.
Anakumbuka baba yake akimtania akiwa mtoto: "Sijali kama hupendi bunduki, kwa sababu ni sheria."
"Nilifundishwa kwamba kama wewe ni mwanaume, unapaswa kumiliki bunduki," anasema.
Sasa ana umri wa miaka 42, na alifyatua risasi ya kwanza akiwa na umri wa miaka 12.
"Nilikaribia kuishusha kwa sababu nilikuwa naogopa sana," anasema Weatherby.
Wakati fulani alimiliki bunduki zaidi ya 20, lakini sasa anasema kwamba hamiliki hata silaha moja.
Aliuza silaha zake kwa miaka mingi ili kujikimu kimaisha, akiwemo ile aliyoachiwa na baba yake alipofariki mwaka 2005.
"Nilihitaji gesi ya kupikia zaidi kuliko bunduki," anasema.
Mahali moja ambapo Weatherby angeweza kupeleka bunduki zake kuuza ni Duka la Silaha la Deercreek, lililopo barabara kuu ya, Kennesaw.
James Raban, mwenye umri wa miaka 36, amefanya kazi katika duka hili la kuuza bunduki tangu alipohitimu kutoka shule ya upili.
Anasema ni biashara ya familia, ilianzishwa na baba yake na babu yake, ambao bado wanapatikana huko leo.
Baba yake hurekebisha bunduki kwenye karakana iliyonyuma ya duka lao, huku babu yake akijibarizi mbele ya duka.
Kwa sababu za dhahiri, Raban ni mpenzi wa sheria ya kumiliki bunduki ya Kennesaw, kwa sababu ni nzuri kwa biashara.
"Kitu kizuri kuhusu bunduki," anasema kwa shauku ya kweli, "ni kwamba watu wanazinunua kwa ajili ya kujilinda, lakini watu wengi wanazipenda tu, kama sanaa au sarafu ya mitandaoni, vitu vya kipekee."
Miongoni mwa mamia ya bunduki zilizoning'inia ukutani na zinazouzwa ni bunduki zenye mapipa mawili, bunduki ndogo, na risasi kadhaa za Winchester za karne ya 19 ambazo "haziundwi tena."

Katika mji wa Kennesaw, wapenzi wa bunduki sio tu wamiliki wa maduka ya bunduki na wanaume wa umri wa kati.
Chris Welch, mama wa mabinti wawili wa vijana, hajionei aibu kumiliki bunduki. Yeye huenda kuwinda, ni mshiriki wa klabu ya bunduki, na hupiga risasi kwenye uwanja wa mazoezi ya kupiga risasi pamoja na binti zake wawili.
"Mimi ni mmiliki wa silaha," anakiri, akitaja silaha zake, ambazo ni pamoja na "bastola ya Ruger, Baretta, Glock, na bunduki zile ndogo."
Hata hivyo, Chris hapendi sheria ya kumiliki bunduki ya Kennesaw.
"Najihisi vibaya ninaposikia watu wakizungumza kuhusu sheria za bunduki," alisema. "Ni mtindo wa zamani ambao Kennesaw inaendelea kuushikilia."
Anataka wageni wa mji wake wavutiwe na mbuga za wanyama, shule, na maadili ya jamii wanapofikiria mji wake, siyo sheria za kumiliki bunduki "zinazosababisha watu kujihisi kutokuwa na raha."
"Kennesaw ni zaidi ya hii sheria," anasema.
Mjumbe wa Baraza la Mji, Madeline Orochena, alikubaliana kwamba "watu wangependa kutoshiriki hadharani" kuhusu sheria hii.
"Ni kama ukweli wa ajabu tu katika maisha ya jamii yetu," anasema. "Watu ama wanageuza macho kwa aibu au wanacheka kuhusu hilo."